Monday, 13 October 2014

MAMA KANUMBA NA LULU NDANI YA FILAMU MPYA IITWAYO "MAPENZI YA MUNGU"


Hivi karibu Msanii Mahiri na Nguli katika tasnia ya filamu nchini Elizabeth Michael almaarufu kama LULU ataibuka na filamu yake Mpya na yenye kusisimua iitwayo "MAPENZI YA MUNGU" ambapo moja kati ya washiriki katika filamu hiyo ni Bi Flora Mtegoha ambae ni Mama Mzazi wa aliyekuwa Msanii Nguli wa Kiume Hapa Bongo Marehemu Steven Kanumba.

Filamu ya "Mapenzi ya Mungu" ni moja ya filamu ambayo Lulu ameonyesha uwezo wa hali ya na kuthibitisha kuwa ni mmoja kati ya wasanii wa kike hapa Tanzania ambae ana kipaji cha hali ya juu katika kuuvaa uhusika ambapo ana uwezo wa kubadilika badilika kutokana na muongozo anaopewa.

Filamu ya "Mapenzi ya Mungu" itakuwa Sokoni hivi Karibu Kwa Wauzaji wa Filamu kote Nchini.

Filamu hii itasambazwa na Kampuni mahiri ya Proin Promotions Ltd.

OFFICIAL MEMBER

OFFICIAL MEMBER

Please Share This Site

HABARI ZETU

LIKE PAGE YETU HAPA