Tuesday, 14 October 2014

WABUNGE DUNIANI WAKUTANA KUJADILI MATATIZO YAKIUSALAMA


Kiongozi wa Ujumbe wa Tanzania katika Mkutano wa 131 wa Chama cha Mabunge Duniani (IPU) Mhe. Hamad Rashid Mohamed akifatilia kwa makini Mkutano wa 131 wa Chama cha Mabunge Duniani (IPU),unaofanyika mjini Geneva,Uswis.

Kiongozi wa Ujumbe wa Tanzania katika Mkutano wa 131 wa Chama cha Mabunge Duniani (IPU) Mhe. Hamad Rashid Mohamed akiteta jambo na Balozi wa Kudumu katika Umoja wa Mataifa Geneva, Uswis, Balozi Modest Mero wakati wa Mkutano wa chama hicho mjini Geneva jana
Ujumbe wa Tanzania ukiongozwa naMhe. Hamad Rashid Mohamed wakishiriki Mkutano wa 131 wa Chama cha Mabunge Duniani (IPU) Mjini Geneva, Uswis.

Na Owen Mwandumbya, Geneva

Wabunge kutoka Mabunge wanachama wa Chama cha Mabunge Duniani (IPU) wanakutana Mjini Geneva Usiwisi katika Mkutano wa mwaka wa 131 wa chama hicho kujadili na kutafuta ufumbuzi wa namna ya kukabiliana na baadhi ya matatizo yanayoyakumba mataifa mbalimbali duniani ikiwemo usalama pamoja na uvunjaji wa haki za Binadamu.


Katika mkutano huo ambao unahudhuriwa na jumla ya wabunge 700 kutoka nchi wananchama 141 wakiongozwa na Maspika na Manaibu spika kutoka nchi 104 umeanza jana tarehe 12 na unatarajiwa kumalizika ijumaa tarehe 16 Oktoba, 2014 kwa kufanya uchaguzi kumchagua rasi wa chama cha kibunge na ambacho ni kikubwa Duniani.

Katika agenda za mkutano huo, mojawapo ya masuala yanayojadiliwa ni pamoja na kuja na suluhu ya kibunge ya namna ya kukabiliana na kubambana na ugaidi duniani na masuala yote ya imani kali yanayopeleka kuleta machafuko katika baadhi ya nchi hususani za kiarabu kwa kuangamiza maelfu ya watu wasio na hatia. Pamoja na masuala hayo, wabunge hao pia wanajadili namna bora ya nchi wanachama kuwa na sheria madhubuti ya kupiga vita biashara haramu ya usafirishaji wa Binadamu, pamoja na kutambua uhuru wa kila Taifa bila kuingiliwa na mataifa mengine.

Tanzania katika Mkutano huo inawakilishwa na Wabunge wambao ni wanacham wa kudumu katika mkutano huo ambao ni mhe. Hamad Rashid Mohamed, Mhe. Suzan Lyimo na Mhe. Dkt. Pudensiana kikwembe.

Katika mchango wa Tanzania, kiongozi wa Msafara wa Wabunge kutoka Tanzania Mhe. Hamad Rashid Mohamed akichangia katika Mkutano mKuu w huo ameelezea namna Tanzania inavyounga mkono jitihada za IPu katika kupiga vita masula ya Ugadi ikiwa ni pmoja na jitihada za chombo hicho kutambua uwakilsihi wa wanawake katika masula ya uongozi.

Akisisitiza umuhimu wa mabunge kuwa na sheria rasmi zinazoweza kumlinda mwananke katika ukatili wa kijinsia, Mjumbe kutoka Tanzania Mhe. Suzan Lyimo amesema, takwimu zilizopo zinaonyesha  kuwa mwananmke mmoja katika kila wanawake watatu hivi sasa ni mhanga wa ukatili wa kijinsia unaofanya katika ngazi ya kifamilia na hata utawala hususani na machafuko ya kivita. Ansema bila kujipanga vyema katika ngazi ya kibunge kuwa na sheria na utaratibu madhubuti ya kumlinda mwananke, machafuko yanayotokea duniani hivi sasa yatazidi kumwangamiza mwanamke .

Akitolea mfano wa makundi hatari yanayotokea duniani hivi sasa kama vile ISIS, BOKO HARAM, ambayo kwa kiasi kikubwa yamekuwa tishio kubwa kwa usalama wa kimataifa bali hata kwa ustawi wa wanawake duniani kutokana na vitendo vyao vya kuwadhalilisha wanawake.

Mkutano huo unaendelea leo kwa kuangalia masula mengine ya kimataifa na namna mabunge yote duniani yatasaidiana na Serikali zake kutatua migogoro hiii ya kimataifa

OFFICIAL MEMBER

OFFICIAL MEMBER

Please Share This Site

HABARI ZETU

LIKE PAGE YETU HAPA