HUU NDIO UJIO MPYA WA VANESSA MDEE NA BARNABA BOY! CHEKI HAPA
Hajafanya kolabo nyingi sana kiasi cha kusema tumezoea, hii ndio sababu nyingine ukisikia V Money ( Vanessa Mdee ) kaungana na msanii mwingine kufanya kazi ya muziki pamoja unakua na hamu ya kuisikia hiyo kazi yenyewe. Hata hivyo haiko mbali na wewe manake November 18 2014 ambayo ni Jumanne wiki hii ndio spika zako zitakupa dakika za hii kolabo inayoitwa siri ambayo inamuhusisha mkali mwingine aitwae Barnaba. @BarnabaClassic