GHANA YAICHAPA TOGO YA ADEBAYOR 3-1, NA KUFUZU AFCON
Pamoja na kucheza bila Gyan Asamoh na Andre Ayew Ghana imefanikiwa kufuzu kucheza fainali za Kombe la Mataifa Afrika (Afcon).
Black Star imefanikiwa kufuzu kwa kuichapa Togo iliyoongozwa na Emmanuel Adebayor iliyokuwa ugenini kwa mabao 3-1, jana.
Kutokana na ushindi huo, Ghana imefikisha pointi 11 na kufuzu katika michuano hiyo mikubwa ya soka Afrika kwa timiu za taifa.
Ghana ilionekana kuizidia Togo kwa kila kitu huku safu ya ushambuliaji ya Ghana ikiichachafya safu ya ulinzi ya wageni.