Tuesday 25 November 2014

KUMBE!!! MTO NGARENARO ARUSHA WATUMIKA KUTUPA WATOTO WACHANGA


Utupaji watoto wachanga katika mto Ngarenaro Mkoani Arusha umekithiri hali inayohatarisha maisha ya wakazi wa maeneo hayo ambayo hutumia maji ya mto huo kwa shughuli zao za kila siku.


Kutokana na hilo wakazi wa eneo hilo hulazimika kufanya usafi mara kwa mara na kulalamikia kukuta miili ya vichanga ambayo hutupwa maeneo hayo kila wakati.

Baadhi ya wakazi hao walisema mto huo ambao chanzo chake kinatoka katika Mlima Meru ni muhimu kwao kutokana na maji yake kutumika kwa matumizi ya nyumbani na hata umwagiliaji wa mboga mboga.

“Unaweza kwenda kuteka maji ukakutana na mabaki ya miili ya watoto huku wengine wakitupa taka kwa kukwepa kulipa ushuru wa takataka ambao ni shilingi 1,000 kwa Halmashauri ya jiji.

OFFICIAL MEMBER

OFFICIAL MEMBER

Please Share This Site

HABARI ZETU

LIKE PAGE YETU HAPA