MESSI AIBEBA BARCA ,AKIVUNJA REKODI YA RAUL
MSHAMBULIAJI Lionel Messi ameifikia idadi ya mabao aliyofunga Raul katika Ligi ya Mabingwa Ulaya baada ya kufunga lake la 71 jana.
Nyota huyo wa Barcelona alifunga mabao mawili dhidi ya Ajax katika ushindi wa 2-0 na sasa anaongoza kwa pamoja na gwiji huyo wa Real Madrid kufunga mabao kwenye michuano hiyo.
Messi, nyota wa vigogo wa Katalunya ili kukamata rekodi hiyo iliyowekwa muongo uliopita, alifunga bao la kwanza kwa kichwa, kabla ya kuongeza la pili kipindi cha pili Barcelona katika mchezo huo wa Kundi F. Pamoja na kushinda, Barca inabaki nafasi ya pili kwa pointi zake tisa, nyuma ya PSG yenye pointi 10 baada ya kuifunga APOEL Nicosia 1-0.