UMESIKIA HII..!! WANAWAKE 600 WAISHIIO KATIKA ENEO AMBALO HALINA WANAUME NCHINI BRAZIL WAOMBA KUPELEKEWA WANAUME
Zaidi ya wanawake 600 wanaotengeneza jumuia ya wakazi katika eneo la women Noiva do Cordeiro kusini mwa Brazil ambao wengi wao wana umri kati ya miaka 20 na 35 wanaomba kupelekewa wanaume kutokana na eneo hilo wanaloishi kutokuwa na wanaume.
Mji huo ambao idadi ya wakaaji wake wote ni wanawake umeomba angalau mwanaume mmoja kwenda kuishi katika eneo hilo ingawa atatakiwa kuishi kulingana na sheria za kike zinazotawala eneo hilo.
Ingawa baadhi ya wanawake hao wameolewa na wanafamilia lakini waume zao hufanya kazi nje ya eneo hilo na wanatakiwa kurudi mwisho wa juma tu (Weekend)
Hata hivyo watoto wa kiume wanapozaliwa na kufikisha miaka 18 wanatakiwa kuondoka na hakuna mwanaume yeyote anayetakiwa kuishi katika mji huo ambao upo umbali wa Mile 60 mashariki mwa Belo Horizonte.
Historia ya eneo hilo inarejea miaka ya 1890 ambapo msichana mmoja na familia yake walitengwa kutoka kanisa la Kikatoliki baada ya kushutumiwa kuwa mzinifu.
Taratibu wanawake wengi ambao walikuwa hawajaolewa pamoja na familia zao walianza kujiunga na jamii hiyo na miongo kadhaa baadae wanaume walifanya majaribio kadha ya kuingia katika eneo hilo hali amabayo ilipelekea jamii hiyo ya wanawake kuanzisha sera ya hakuna mwanaume "'no male' policy."
Mmoja wa wanawake hao aliyefahamika kwa jina la Nelma Fernandes mwenye maiaka 23, anakili kwamba ni vigumu kwa msichana anayejulikana katika hilo eneo na ni mrembo kuacha kuchumbiwa ikiwa mwanaume atamuona ila tatizo ni ukosefu wa wanaume hao.
Anasema "mwanaume pekee ambao wasichana hutana nao ni wale ambao wameoa au wana uhusiano wa kindugu,Wote ni binamu.Nimembusu mwanaume muda mrefu sana uliopita."
Anaongeza kusema kuwa "Wote tunandoto ya kupenda na kuolewa lakni tunapenda kuishi hapa na hatutaki kwenda mjini kutafuta wanaume."