Saturday, 15 November 2014

ZIJUE SABABU MUHIMU ZINAZOMPELEKEA MWANAMKE KUKOSA BAHATI YA KUOLEWA,PART TWO


Pamoja na kuwa kuna wanawake husita kuolewa, lakini jambo hili si kubwa sana kwa wanawake kama ilivyo kwa wanaume.
Kwa kiasi kikubwa katika suala la kutaka kuingia ndani ya ndoa, wanawake ni wengi ambao hutaka kufunga ndoa kuliko ilivyo kwa wanaume. Hilo tunaliona wazi tokana na shamra shamra awazo nazo mwanamke wakati wa maandalizi ya shughuli za Ndoa na Harusi.
 



Hata hivyo, kwa wale wanawake wachache ambao husuasua kuolewa hizi ni baadhi ya sababu zinazopelekea kusuasua huko. (Izingatiwe hii ni kwa wanawake ambao hawajawahi kuolewa kabisa)
6. Kujiona ana Umri mdogo
Binti yeyote wa miaka 18 na kuendelea anaruhusiwa kuolewa endapo tu karidhia kuolewa.
Wanawake wametofautiana mipangilio yao ya kimaisha, kuna wale akiwa katika umri wa kuolewa hutamani sana kuolewa na kuna wale ambao hupenda kuolewa wakiwa wakubwa zaidi.
Katika kundi hili umri kuwa mdogo hutegemeana, kuna mwingine anakuwa na umri wa miaka 25 na bado akajiona mdogo na hali kuna mwingine anakuwa na miaka 20 na akajiona ni mkubwa na anafaa kuolewa.
Hii pia ni kwa wanawake wale ambao huwa na malengo ya kutotaka kuharakisha katika ndoa.
Anapokuwa na umri ambao anaweza kuolewa lakini yeye hayupo tayari kwa muda huo, huwa ni kikwazo kwake kuingia katika ndoa.

7. Maradhi hasa UKIMWI
Hili kama lilivyo kwa wanaume - Pamoja na kuhamasishwa kwingi na wataalamu wa maradhi ya HIV/AIDS kuwa mtu hata ukiwa umeathirika unaweza kuwa na mahusiano na hata kuoa na kuwa na watoto; bado haisaidii sana kwa vijana wanaojitambua kuwa ni waathirika wakiwa bado ni wadogo, hawajaoa/olewa ama kuwahi kuwa na mtoto.
Wengi sana hukata tamaa na huona ni kheri kubaki walivyo kuliko kuingia katika ndoa, hasa tokana na imani kuwa wanawake wakizaa wakati ni waathirika; afya hudhoofika zaidi.

8. Kutaka maisha ya Tamthilia (Ndoa za kuishi kwa furaha milele)
Kutokana na kukua kwa idadi ya tamthilia nyingi ambazo huonyesha maisha ya kimagharibi zaidi; kumekuwa na dhana kwa baadhi ya wanawake kutaka hayo maisha ya tamthilia yawe na kwao pia.
Hilo linafanya vigezo ambavyo mwanamke huyo anatumia kuchagua ama kukubali mwanaume kumuoa kutotimiza yale ambayo yeye binafsi anatarajia.
Wengi hushindwa kutambua kuwa hakuna maisha ya furaha milele, na hasa kuwa maisha ya maigizo yapaswa kuchanganya na zako kuweza kufanya maamuzi ya kipi kiigwe na kipi kiachwe kama kilivyo.
9. Kuona taasisi ya Ndoa kama Utumwa
Mtazamo huu kwa wanawake wenye msimamo huu, huchangiwa na baadhi kama haya:
- Usomi: Aina ya usomi ambao hupelekea kwa baadhi kuwa na tafsiri tofauti juu ya ndoa, haki, majukumu na mengine mengi.
- Kushuhudia ndoa mbovu: Hii inaweza kuwa ya wazazi/walezi wake wenyewe (pengine mama aliteswa sana), na hata ndugu wa karibu kama vile kushuhudia kila ndoa ya ndugu yake anayoijua mwanamke huishi kwa mateso, manyanyaso na maisha ya taabu na kuonewa.
- Kuwa na uwezo sana wa kujitosheleza ambao unaweza kumtimizia na kufanya lolote lile ambalo anataka katika maisha. Kwake kuwa na mwanaume kama mume kwake anaona kama ni utumwa.
10. Kutokuwa kabisa na mshipa wa hisia za kufanya mapenzi
Kuna wanawake wale wachache waliozaliwa hivyo. Hawana hisia yoyote ile ya kimwili ya kuweza kupata hisia za kuweza kujisikia ama kutamani kufanya mapenzi.
Wengi wa aina hii ya wanawake huwa ni waoga sana wa kuwa karibu na mwanaume, na kwa wale ambao wamewahi hata jaribu baadhi huona kama kitendo cha ndoa ni kero, unyanyasaji na uchafu.
Hivyo wazo la kuwa akiolewa anatarajia kufanya kitendo cha ndoa mara kwa mara kinamvunja kabisa hamu ya kutaka kuolewa.

OFFICIAL MEMBER

OFFICIAL MEMBER

Please Share This Site

HABARI ZETU

LIKE PAGE YETU HAPA