Friday, 15 September 2023

UNATAKA KUOA ALIYEEFIWA NA MUME? SOMA HII UJUE PAKUANZIA



Katika jarida la Health Psychology la hivi karibuni linaripoti kwamba, mwanamke akifiwa na mumewe, kama walikuwa wakipendana sana, basi kwa muda wa mwaka mzima mwanamke huyo anakuwa katika hali ya tatizo la kiakili. Ni baada ya mwaka mmoja, ndipo ambapo hali yake inaanza kurudi katika hali yake ya kawaida. 
Kwa hiyo kama mwanaume anataka kuoa au kuwa na uhusiano na mwanamke aliyefiwa na mumewe, anapaswa kuvuta subira ipite angalau miaka mitatu kabla hajafanya hivyo, kwani akiwahi, anaweza kujikuta anaishi na “Kichaa” na akamwona kwamba, hafai. Kichaa hiki kinatokana na sababu mbalimbali baada ya mwanamke kufiwa. 
Mabadiliko ya kihisia ambayo husababishwa na hofu ya upweke, huzuni, maswali yasiyo na majibu kuhusu mustakabali wa maisha, kujilaumu kwa namna fulani na simanzi kwa ujumla, humfanya mwanamke kuingia kwenye aina ya kichaa cha kimya kimya. 
Kwa kawaida, wanawake wa umri wa kati ya miaka 30 hadi 50 wanapofiwa na waume, kama walikuwa wanawapenda, huingia katika sononi kuu, hushindwa kukabili masuala mengi ya kijamii ambayo awali walikuwa wanaweza kuyakabili na pia kupata hata matatizo ya kimwili ambayo mara nyingi ni maradhi. 
Wanawake wanaofiwa na waume zao nao wanashauriwa kukaa kwa zaidi ya mwaka mmoja bila kuanzisha uhusiano na wanaume wengine kwa sababu, wakifanya hivyo, uwezekano wa uhusiano huo kuvunjika ni mkubwa, kwani akili zinakuwa hazijatulia. 
Hata hivyo, kama mwanamke alikuwa anampenda mumewe, inakuwa vigumu kwake kuanzisha uhusiano kabla ya mwaka mmoja kupita. 
Siyo kufiwa, bali hata kuachana. Mwanamke au hata mwanaume anapoachana na mpenzi wake hatakiwi kukurupuka kuanzisha uhusiano mwingine. Kama alikuwa anampenda sana mpenzi waliyeachana ni wazi ataumia kiakili kwa muda mrefu na hivyo kuanzisha uhusiano mpya mapema, kunaweza kumdhuru zaidi. Kumdhuru zaidi kwa sababu akili yake inakuwa haijatulia.

OFFICIAL MEMBER

OFFICIAL MEMBER

Please Share This Site

HABARI ZETU

LIKE PAGE YETU HAPA