BREAKING NYUZZZZ..YANGA YAIFANYIA SIMBA UMAFIA...: YAMSAJILII DANNY MRWANDA
10:11 |
No Comments |
Mshambuliaji Danny Mrwanda amemwaga wino wa kuitumikia klabu ya Yanga ya jijini Dar es salaam kwa mkataba wa mwaka mmoja usiku huu.
Yanga imewafanyia umafia watani zao wa jadi Simba,ambayo ilionyesha nia kubwa ya kumuhitaji Mrwanda ikiwa ni kwa hudi na uvumba na tayari ilishatangaza nia yake hiyo ya kutaka kumsajili.
Chanzo cha kuaminika kutoka ndani ya Klabu ya Yanga kinasema kuwa,Yanga imeamua kumsajili Mrwanda kuchukua nafasi ya Said Bahanuzi aliyetolewa kwa mkopo kwenda Polisi Morogoro wakati Jerry Tegete akiwa ni majeruhi,na mshambuliaji pekee wa ndani wanayemtegemea ni Hussein Javu.

Mrwanda kutua Yanga SC ni kutimia kwa ndoto zake, kwani wakati anachipukia kisoka aliwahi kwenda kufanya majaribio ya kuomba kusajiliwa, lakini hakufanikiwa mwaka 2005 na karudi AFC ya Arusha.
Mrwanda, mwenye umri wa miaka 31 sasa, aliibukia AFC ya mwaka mwaka 2003 ambako alicheza hadi 2006 alipohamia Simba SC alikocheza hadi 2009 alipokwenda Al Tadamon ya Kuwait.
Alirejea Simba SC mwaka 2009 na akacheza hadi 2010 alipokwenda Vietnam kujiunga na Dong Tam Long An ambayo aliichezea kwa msimu mmoja kabla ya kuhamia Hoang Anh Gia Lai aliyochezea hadi mwaka huu alipojiunga na Polisi Morogoro.
Baada ya kusaini Mkataba huo, usiku huu Mrwanda anakwenda kujiunga na wachezaji wenzake katika hoteli ya Landmark, Mbeazi Beach kwa maandalizi ya mechi ya Nani Mtani Jembe dhidi ya Simba SC Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Related Posts:
MESSI AIZAMISHA ARSENAL UWANJA WA EMIRATES Mshambuliaji wa Barcelona, Lionel Messi akikimbia kushangilia baada ya kuifungia timu yake bao la kwanza. Anayemfuata ni mchezaji mwenzake, Lui… Read More
UEFA: CRISTIANO , JESSE WAIONGOZA MADRID KUINYUKA AS ROMA NYUMBANI Mshambuliaji wa Real Madrid, Cristiano Ronaldo akiugulia maumivu baada ya kuchezewa rafu na Radja Nainggolan wa AS Roma katika mchezo wa kwanza ha… Read More
JESHI LA POLISI::ULINZI UTAKUWA WA UHAKIKA MECHI YA WATANI WA JADI Kamishina wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, CP. Simon Sirro a… Read More
ULIMWENGU: NILICHEZA KIBISHI BISHI TU SUPER CUP, MGUU ULIKUWA UNAUMA ILE MBAYA Na Mwandishi Wetu, LUBUMBASHI MSHAMBULIAJI wa kimataifa wa Tanzania, Thomas Emmanuel Ulimwengu amesema kwamba alicheza mechi ya kuwania Super Cup … Read More
JUVENTUS YASHIKWA SHATI NA BEYERN MUNICHENBayern Munich imelazimisha sare ya 2-2 na wenyeji Juventus Uwanja wa Juve. Kiungo wa Juventus, Paul Pogba (kushoto) akimtoka Nahodha wa Bayern Muni… Read More
0 comments:
Post a Comment