SEHEMU YA KWANZA::NAMNA YA KUONDOA MSONGO WA MAWAZO NA MFADHAIKO
Mara nyingi sana umesikia mtu akisema “nina stress”, mwingine
akasema ana msongo wa mawazo na mara chache katika mazungumzo ukasikia mtu
akitumia neno mfadhaiko. Haya ni maneno yanayoingiliana kimazungumzo
mitaani na mara nyingi mtu hutumia neno moja katika hayo bila kujua tofauti
zake. Katika mada yetu tutayachambua na kujua tofauti za matatizo
yanayowasumbua watu hadi kupelekea kuyatumia maneno haya. Na mwisho
tutatoa ushauri wa namna ya kuondokana na matatizo hayo.
Kwa Kuanza Tuangalie Maana Ya Stress Au Msongo Wa Mawazo
Maisha ya dunia ya leo yamejaa
pilikapilika za kila aina, una vitu vingi vya kuvifanya katika
muda uliopangiwa (deadlines), vitu vingi vya kukukatisha tamaa na matakwa
mengi ya binafsi na watu walio karibu na wewe. Mtindo huu wa kuishi
umekuwa karibu ni wa kila mtu. Kila wakati unakuwa na msongo wa
mawazo (Stress).
Msongo wa mawazo kwa kiasi fulani siyo mbaya, unakusaidia
kutekeleza majukumu yako ukiwa umebanwa na kukupa nguvu ya ziada ya
kuyafanya vizuri kadiri ya uwezo wako. Lakini kama utaendelea kufanya
shughuli zako kwa mtindo huu, wakati utafika ambapo ubongo wako utachoka
na kupata tatizo la kiafya linaloitwamfadhaiko (Depression).
Kwa
hiyo msongo wa mawazo (Stress) ni namna ya kawaida ya mwili wako kukabiliana na
mambo ya kukutisha au kukufanya uwaze.
Unapohisi
hatari, ya kweli au siyo ya kweli, mwili hukupa nguvu haraka kukabilina na
suala lililopo mbele yako, hii ni ni namna ya mwili wako kukulinda. Katika
mazingira hayo, mwili hukufanya uwe mwangalifu zaidi na kukupa nguvu ya
ghafla.
Katika mazingira ya hatari, unaweza kuokoa maisha yako kwa kupata
hiyo nguvu na ujasiri wa ghafla. Mfano mzuri ni pale unapoendesha gari na
ghafla ukakanyaga breki za gari kuzuia ajali mbele yako.
Msongo
wa mawazo hukusaidia kukabiliana na vikwazo mbalimbali. Utakuwa makini sana
wakati unawasilisha mada mbele ya kadamnasi, utakuwa na umakini zaidi
wakati unashiriki kwenye mechi na timu pinzani na utasukumwa kwenda kusoma
ili ujiandae kwa mitihani yako badala ya kuangalia kipindi kizuri
cha kwenye luninga unachokipenda.
Lakini
kama tulivyodokeza hapo awali, kiwango cha msongo wa mawazo kikizidi, badala ya
kukusaidia kitakuletea matatizo ya afya, kitaathiri utendaji wako wa kazi,
kitavuruga mahusiano yako na wengine na kudunisha maendeleo yako ya
maisha.
USIKOSE SEHEMU YA PILI
credit: topantiagingproducts
0 comments:
Post a Comment