Friday 26 December 2014

CHELSEA YAUA YAJIKITA KILELENI.



Costa scored on the hour as he fired into the far corner beyond West Ham goalkeeper Adrian to double Chelsea's lead at Stamford Bridge

Costa akiifungia bao la pili Chelsea Uwanja wa Stamford Bridge

TIMU ya Chelsea leo imeshinda mechi ya tatu mfululizo ya Ligi Kuu ya England baada ya kuichapa West Ham United mabao 2-0 Uwanja wa Stamford Bridge, London.

Beki na Nahodha, John Terry aliifungia Chelsea bao la kwanza dakika ya 31 akimalizia kazi nzuri ya mshambuliaji Diego Costa.
Diego Costa mwenyewe akafunga bao la pili dakika ya 62 akimalizia pasi ya Eden Hazard, kabla ya kumpisha mkongwe Didier Drogba dakika ya 83.
Chelsea imefikisha pointi 45 ikiwa kileleni kwa tofauti ya pointi 3 dhidi ya Manchester City ambayo nayo imeichapa Westbromich Albion goli 3 kwa moja.

0 comments:

Post a Comment

OFFICIAL MEMBER

OFFICIAL MEMBER

Please Share This Site

HABARI ZETU

LIKE PAGE YETU HAPA