EXCLUSIVEEE!!!!HIZI NDIO FAIDA 5 ZA KUNUNIANA NA LOVE WAKO !
YAWEZEKANA kuwa ni mada ambayo imekuachahoi mpenzi msomaji wangu huku ukijiuliza kama ni kweli zipo faida kwa watu wanaopendana kwa dhati kununiana.
Faida ipi hiyo zaidi ya maumivu na mateso ya moyo? Jamani ni kweli kabisa kwamba kuna maumivu na karaha nyingi unaponuniana na mpenzi wako, lakini wakati huo huo kuna faida nyingi za kununiana naye. Mapenzi yana wigo mpana mno ambao mtu anapaswa kuuangalia kwa jicho pana na akili pembuzi kabla ya kuingia,namaanisha kwamba ni lazima kuchunguza kina cha maji kabla ya kuzamia. Sasa basi, zifuatazo ni faida tano utakazozipata ukiwa umenuniana na mpenzi wako.
HUSAIDIA KUPUNGUZA MIGOGORO
Ni ukweli usiopingika kuwa, katika hali ya kawaida, ukiwa mbali na mtu fulani katika jamii unayoishi ni vigumu sanakujikuta umekwaruzana naye. Hii ni kwasababu utakuwa hauingiliani nayekatika mizunguko yako, vivyo hivyo kwa wapenzi walionuniana.Hali hii hupunguza kabisamigogoro ya hapa na pale, kwani hiki ni kipindi ambacho mtakuwa mbalimbali jambo ambalo huepusha maudhi ya kibinadamu.Mfano, yawezakana katika kipindi mlichonuniana na mpenziwako, uliingia ujumbe wa mapenzi kwenye simu yake kutoka kwa mtu aliyekosea namba. Kwa kuwa hauko naye karibu jambo hili halitakuumiza maana hutaelewa nini kimeendelea tofauti na kama ungelikuwa naye karibu.Kwa hiyo kuna baadhi ya maumivu na maudhi ambayo utaepukana nayokwa kipindi cha kununiana kwenu. Ni kweli kabisa kwamba hupunguza migogoro na mitafaruku ya hapa na pale, umeelewa mpenzi msomaji wangu? Haya twende kwenye faida ya pili.
KUBAINI TABIA ZA MWENZAKO
Hiki ni kipindi ambacho sasa kitakusaidia wewe kubaini tabia na mienendo mibaya ya mwenzi wako. Hii ni kwa kuwa utakuwa mbali naye hivyo naye hujiona kuwa yuko huru kufanya jambo lolote analoona kuwa linafaa bila kujali uwepo wako kwani kila mtu ana ‘time’ na mwenzake.Kama kuna asili ya maisha yake ambayo aliiacha baada ya kuingia katika uhusiano na wewe,ambayo ni mbaya zaidi sasa hapa ataanza kuirudia kwa kujiona kuwa hana mtu wa kumzuia na kumbana.Kama ni mlevi kupindukia,mchafu, muongo na tabia nyingine mbaya za kufanana na hizi basi ataanza kuzionesha katika kipindi ambacho mmenuniana.
KUPATA MUDA WA KUTAFAKARI ZAIDI
Hapa naomba nieleweke vizuri kabisa kwamba, ninapoongelea suala la kutafakari zaidi katika kipindi ambacho wewe hauna maelewano mazurina mwenzi wako, namaanisha kuwa utapata muda mzuri zaidi wa kutafakari penzi lenu kwa ujumla.Ni kipindi kitachokuongoza wewe kuwa na uelewa wa ni aina gani ya mpenzi uliyenaye. Kivipi? Ni kwamba, katika muda huu mara nyingi utataka kupata suluhu ya kununiana kwenu, lakini pia katika kutafuta suluhuhiyo utapata fursa ya kutafakari kwa kina juu yapenzi lenu huku ukimpima mwezi wako kwa mtazamo chanya.
KUFAHAMU AINA YA MARAFIKI ZAKE
Si kila rafiki wa mwenza wako ana nia nzuri na uhusiano wenu au anafurahia penzi lenu. Mathalani, labda wewe ni msichana na pengine miongoni mwa rafiki zakekuna mmoja au wawili ambao hutamani sana kupata penzi lako.Sasa katika kipindi ambacho utakuwa umenuniana na mpenzi wako basi itakuwa ni nafasi nzuri kwao kuitumia kunyunyizia sumu ya kumponda huku wakikutamkia maneno ya kukushawishi, hivyo utakuwa umeelewa ni aina gani ya marafiki alionao mwenzi wako.Hii si kwa msichana tu, hata kwa wanamume kwani huenda kati ya rafiki wa ‘girlfriend’ wako, kuna wanaokutamani, sasa wakiona huna uhusiano mzuri na mpenzi wako, watatumia nafasi hii kukuambia maneno ya uongo juu yake na kukuonesha kila dalili za kukutaka.Hivyo utakuwa umefahamu ni aina gani ya rafiki ambao mpenzi wako anao. Tambua kwamba, marafiki wengi wana tabia zinazofanana.
KUBAINI AINA YA PENZI ALILONALO KWAKO
Katika kipindi hiki, utaweza kuelewa ni aina gani ya penzi alilonalo huyo mtu wako juu yako. Kwa mpenzi aliye na hisiaza dhati kabisa kwako, katika kipindi hiki atakuwa ni mtu wa kutafuta njia ya kupata suluhu ya tatizo lenu.Pamoja na kwamba wewe utakuwa umenuna, bado yeye ataonesha kukujali kama kawaida, atakupigia simu za hapa na pale yaani ilimradi tu asikie angalau sauti yako,lengo lake likiwa ni kutaka kurejesha ukaribu ambao sasa anaona kama akiupoteza itakuwa ni maumivu kwake.Kwa mantiki hiyo basi, utagundua ni kwa jinsi gani anathamini penzi lenu na ni aina gani ya penzi alilonalo kwako. Yote haya utabahatika kuyajua kupitia kipindi cha kununiana kwenu.Hata hivyo, niwatahadharishe kwamba, kuandika haya isiwe ni tiketi ya wewe sasa kuanza kununiana na mpenzi wako eti kwa kigezo kwamba utapata nafasi ya kumfahamu, la hasha! Siku zote katika uhusianowako epuka maudhi na migogoro isiyokuwa ya maana.