Wednesday 31 December 2014

SIMBA WAMTIMUA KOCHA WAKE PATRICK PHIRI


Phiri
Baada ya Yanga kumfungashia virago kocha Mbrazil, Marcio Maximo, mahasimu wao wa Simba nao wamemtimua kocha wake, Mzambia Patrick Phiri.Hatua hiyo imekuja siku chache tu baada ya Simba kufungwa bao 1-0 kwenye mechi ya ligi kuu Tanzania bara. Phiri amesema amepokea taarifa za kusimamishwa kwake na amedai kuwa amesikitishwa lakini hana kinyongo na uongozi wa klabu hiyo.“Wamenitaarifu kuhusiana na kuachishwa kazi, hili si jambo jipya, ingawa niliona tungeweza kubadilisha mambo,” amesema. “Najua Simba wanataka kufanya vizuri, hivyo siwezi kumlaumu mtu na utaona mwendo wa timu yetu ulivyokuwa.”
Taarifa zinadai kuwa nafasi yake itachukuwa na kocha Mserbia, Goran aliyewahi kuifundisha polisi ya Rwanda na atasaidiwa na Jean Marie Ntagawabila wa Rwanda

0 comments:

Post a Comment

OFFICIAL MEMBER

OFFICIAL MEMBER

Please Share This Site

HABARI ZETU

LIKE PAGE YETU HAPA