Wednesday 21 January 2015

CHELSEA CHUPU CHUPU KUZAMA ANIFIELD YATOKA SARE NA LIVERPOOL


Hazard akishangilia bao alilofunga kwa mkwaju wa penati
Katika nusu fainali ya kwanza ya Kombe la Capita one Chelsea iliifuata  Liverpool uwanja wa Anifield na kutoka sare ya kufungana goli mija kwa moja.
Katika mchezo huo ambao kwa kiasi kikubwa ulitawaliwa na soka la kupendeza na vijana hao wa Liverpool ilishudia Chelsea ikipata bao la kuongoza katika dakika ya 16 kufuatia mkwaju wa penalt baada ya Eden Hazard kuangushwa na Emre Can goli liliofungwa na Eden Hazard mwenyewe na kudumu hadi mapumziko.


Katika kipindi cha pili Liverpool walizidi kulisakama lango la wapinzani wao lakini walionesha ubutu katika eneo la umaliziaji jambo lililowanyima nafasi kadhaa za kupata mabao mengi ingawa uimara wa kipa wa Chelsea uliibeba Chelsea.
Katika dakika ya 70 Raheem Sterlin aliweza kuipepeta ngome ya Chelsea na kufunga goli zuri ambalo liliamua hatima ya mchezo huo ambao ulipambwa na mbwembwe za nahodha wa Liverpool Steven Gerad kwa aina ya pasi alizokuwa akipiga.




Mchezo wa marudiano utapigwa wiki ijayo katika uwanja wa Stamford Bridge.
leo itachezwa Nusu fainali ya pili ambapo Totenham Hotspurs itakapoikaribisha Shefield United katika uwanja wa Whiteheart Lane.

0 comments:

Post a Comment

OFFICIAL MEMBER

OFFICIAL MEMBER

Please Share This Site

HABARI ZETU

LIKE PAGE YETU HAPA