Wednesday 28 December 2016

ETI HAKUNA MWANAUME ANAYEWEZA KUDUMU NA MWANAMKE MMOJA...SOMA HAPA


Kwa wale nitakaowakwaza naomba mniwie radhi lakini kiukweli hata mimi hainipendezi kuyasema haya ila ni vema tu niwaeleze dada zangu kwasababu ukweli unaoumiza ni bora kuliko uongo unaofurahisha. Hakuna mwanaume lijali anayeweza kuwa na mwanamke mmoja, eidha awe ameoa au hata kama hajaoa.

Image result for arguing black couples Hakuna mwanaume wa aina hiyo kwa karne hii, usijidanganye kukimbilia kwenye ndoa ukiamini kwamba baada ya kuolewa utajimilikisha huyo mwanaume aliyekuoa, never! "Mchele mmoja mapishi mbalimbali", utakuta ww mwanamke kila siku ukikutana na jamaa yako faragha lazima yeye ndio aombe kamchezo, wakati kuna sehemu akienda mwanamke mwenzako ndio anaandaa mazingira ya kuomba kamchezo kutoka kwa jamaa, now u see the difference? Au mara zote mkitoka lazima wewe ndio uwe ume suggest mtoke tena yeye ndio ana pay bills, wkt kuna mwanamke mwenzio somewhere ingawa sio mara zote, ila mara chache chache yeye ndio anamuomba jamaa watoke na ndio ana pay bills, umeona?

Humshauri jamaa hata kununua an asset, wewe ni kuvaa na kujirusha wkt kuna mwanamke mwenzako kashatafuta kiwanja kwa siri huku mkononi ana angalau robo amount ya gharama nzima ya kiwanja, upo hapo? Kwa mliooana, mumeo karudi home, hata kabla hujampokea ni makelele mtindo mmoja, 
Unaleta mere allegations kwamba anakusaliti wakati hujathibitisha, yani mawivu yako tu yanakuwehusha, wakati kuna mwanamke mwenzio jamaa akienda kwake anapokelewa kwa utulivu, anaenda kuogeshwa tena kwa maji yenye iriki, anakula chakula tena kile anachokipenda, anakandwa apunguze uchovu then anapumzishwa, unaona hapo? Dada zangu yani hakuna mwanaume anayeweza kuwa na mwanamke mmoja coz hawezi kuwa na vyote ambavyo wanaume tunavihitaji. Sihubiri michepuko iendelee ila hiyo ndio hali halisi, angalau mjitahidi kuwa mnasoma alama za nyakati ili angalau apunguze michepuko na ikibidi aache kabisa.

Hapa ngoja nikuweke sawa, mwanamke anayejua nini maana ya mapenzi na namna mwanaume anav yokuwa handled ataweza kumtuliza na Hakika hata salitiwa ,vile vile wanaume wanaojua kwamba mapenzi ni kitandani tu,au pesa tu, au simu tu.....nao nawapa pole kwani watasalitiwa..Kila mmoja acheze katika nafasi yake na tutaipata ile furaha ya kweli.

Lakini pia kuzungumza na mwenzio iwe tamaduni yenu maana hadi mwenza wako anakusaliti huenda hakina nafasi ya ninyi kukaa na kuelezana yale yanayowasibu,ni vyema mkapeana nafasi na kuepusha woga MSISHUTUMIANE kila mmoja wenu awe tayari kupokea na kusikiliza kisha kutendea kazi yale matakwa ya mwenzie maadam hayana athari hasi katika maisha yenu ya kimwili na kiroho pia.

0 comments:

Post a Comment

OFFICIAL MEMBER

OFFICIAL MEMBER

Please Share This Site

HABARI ZETU

LIKE PAGE YETU HAPA