Thursday 29 December 2016

LIGI KUU UINGEREA::SPURS YAIZAMISHA SOUTHAMPTON NYUMBANI

Dele Alli ametikisa nyavu mara mbili wakati Tottenham wakiendelea kuisaka nafasi ya nne ya msimamo wa Ligi Kuu ya Uingereza, baada ya kuifunga Southampton magoli 4-1.

Southampton walikuwa wa kwanza kupata goli katika dakika ya pili ya mchezo kupitia kwa beki
Virgil van Dijk, lakini Dele Alli alisawazisha katika dakika ya 19.

Harry Kane alimaliza ukame wa kutofunga goli katika michezo mitatu kwa kufunga goli la pili, naye Son Heung-Min akaongeza la tatu huku Alli akimalizia goli la nne.
               Harry Kane akiruka juu na kuupiga kwa kichwa mpira wa kona uliozaa  goli

                               Son Heung-Min aliyetokea benchi akifunga katika mchezo huo

0 comments:

Post a Comment

OFFICIAL MEMBER

OFFICIAL MEMBER

Please Share This Site

HABARI ZETU

LIKE PAGE YETU HAPA