Friday 9 January 2015

RAISI MPYA SRI LANKA KUAPISHWA LEO


Rais mpya wa Sri Lanka Maithripala Sirisena anatarajiwa kuapishwa baadaye leo.
Hatua hiyo inakuja baada ya Rais anayemaliza muda wake, Mahinda Rajapaksa kukubali kushindwa katika uchaguzi mkuu uliofanyika Alhamisi.
Amekubaliana na ushindi alioupata mpinzani wake katika uchaguzi huo. Kiongoazi huyo mpya Maithripala Sirisena aliwahi kuwa waziri katika serikali ya nchi hiyo.
Msemaji wa Rais wa Sri Lanka amesema Bwana Rajapaksa ameondoka katika makaazi ya Rais na atahakikisha anayakabidhi madaraka kiutaratibu.
Baada ya kutangazwa kushindwa kwa Rajapaksa fataki zilipigwa maeneo mengi ya nchi . Aliitisha uchaguzi mapema kwa matumaini ya kulinda nafasi yake ya kukaa madarakani kwa awamu ya tatu.
-BBC

0 comments:

Post a Comment

OFFICIAL MEMBER

OFFICIAL MEMBER

Please Share This Site

HABARI ZETU

LIKE PAGE YETU HAPA