Monday 9 February 2015

LIGI KUU NCHINI UINGEREZA, CHEKI JINSI MANCHESTER UINTED ILIVYOBANWA NA WEST HAM



Manchester United ikicheza ugenini imejikuta ikitoka uwanjani ikiwa imefungana bao 1-1 na wenyeji wao West Ham United katika mchezo wa ligi kuu nchini Uingereza hapo jana. 

Matokeo hayo yameifanya Man U kufikisha pointi 44 ikiwa katika nafasi ya nne katika msimamo wa ligi hiyo. 

Cheikhou Kouyate aliifungia West Ham bao la kuongoza kabla ya Daley Blind haijaiswazishia Manchester United bna kufanya matokeo kuwa 1-1.
Yenyewe Newcastle ikicheza nyumbani ilishindwa kuibuka na ushindi wa pointi tatu baada ya kujikuta ikilazimishwa sare ya kufungana bao 1-1 na Stoke City. 

Jack Colbackaliifungia Newcastle bao la kuongoza lakini Peter Crouch aliisawazishia Stoke kwa bao safi la kichwa na kufanya matokeo hadi mwisho wa mchezo kuwa 1-1.Katika mchezo mwingine wa ligi kuu nchini Uingereza hapo jana kati ya Burnley na West Brom ulimazikia kwa timu hizo kufungana mabao 2-2. 

Mabao ya Burnley yalifungwa na Ashley Barnes katika dakika ya 10 na bao la pili likafungwa na Danny Ings katika dakika ya 32. 

West Brom mabao yake yalifungwa na Chris Brunt kunako dakika ya 45 na baadaye Brown Ideye akafunga bao la kusawazisha katika dakika ya 67.

0 comments:

Post a Comment

OFFICIAL MEMBER

OFFICIAL MEMBER

Please Share This Site

HABARI ZETU

LIKE PAGE YETU HAPA