Sunday, 8 February 2015

LIGI KUU UINGEREZA, CHELSEA HAIKAMATIKI, ARSENAL HOI, MANCHESTER CITY ,LIVERPOOL WABANWA UGENINI



Nafuta kiatu chako wewe ni shujaa wetu. Mchezaji wa Chelsea, William ( aliyepiga goti ) akifuta kiatu cha Ivanovic baada ya kufunga goli safi la pili nala ushindi kwa matajiri hao wa London. 

Timu ya soka ya Chelsea imeendelea kuongoza ligi kuu nchini Uingereza kwa kufikisha pointi 56 baada ya jana kuitandika nyumbani kwao Aston Villa mabao 2-1. 

Hata hivyo ushindi haukuwa rahisi kwa Chelsea kutokana na soka safi lililoonyeshwa na Villa waliokuwa wakifanya mashambulizi ya mara kwa mara langoni mwa wageni wao. Magoli ya Chelsea yalifungwa na Eden Hazard dakika ya 08 na Ivanovic dakiak ya 66.
Katika mchezo mwingine wa ligi kuu nchini Uingereza hapo jana Arsenal walishindwa kulilinda goli walilokuwa wametangulia kulipata dhidi ya Tottenham na kujikuta wakifungwa mabao 2-1. 

Wkicheza katika uwanja wao wa nyumbani wa White Hart Lane, Tottenham waliwabana Arsenal na kufanikiwa kuibuka na pointi 3. 

Bao la utangulizi la Arsenal lilifungwa na Ozil katika dakika ya 11, kabla ya Tottenham kusawazisha katika dakika ya 56 kupita kwa Kane ambaye alifunga tena bao la pili nala ushindi katika dakika ya 86.
Wao Liverpool wakicheza ugenini walishindwa kutamba mbele ya Everton na kulazimishwa sare butu ya kutofungana baada ya kumaliza dakika tisini ubao wa matokeo ukisomeka 0-0.
Mabingwa watetezi wa kombe hilo, Manchester City walifanya kazi ya ziada kukomboa bao walilotanguliwa kufungwa na Hull City waliokuwa nyumbani. 

Hull walipata bao la katika dakika ya 35 mfungaji akiwa ni David Meyler. Bao la kusawazisha la Man City lilifungwa na James Milner baada ya mpira wa adhabu aliopiga kwenda moja kwa moja kimiani.
Swansea na Sunderland nazo zilijikuta zikigawana pointi moja moja baada ya kumaliza mchezo wao timu hizo zikiwa zimefungana bao 1-1. 

Katika mchezo huo wa ligi kuu Uingereza, wageni Sunderland ndio waliokuwa wa kwanza kupata bao kupitia kwa Jermain Defoe aliyefunga katika dakika ya 42. Bao la kusawazisha la wenyeji lilifungwa na Ki Sung-yueng dakika ya66.
Bao kutoka kwa Ledley katika dakika ya 55 kipindi cha pili cha mchezo lilitosha kuwapa ushindi Crystal Palace waliokuwa wakicheza ugenini dhidi ya Leicester katika mchezo mwingine wa ligi kuu nchini Uingereza hapo jana.
Southampton wameendelea kuimarika katika ligi kuu nchini Uingereza na kusimama katika nafasi ya tatu wakiwa na pointi 45 baada ya jana kuifunga QPR bao 1-0 katika mchezo wa ligi kuu nchini humo. 

Bao safi lililofungwa na Mane katika dakika za mwisho wa mchezo lilitosha kuwafanya Southampton kujiimarisha na kujikita katika nafasi ya tatu.
-Rweyunga blog

0 comments:

Post a Comment

OFFICIAL MEMBER

OFFICIAL MEMBER

Please Share This Site

HABARI ZETU

LIKE PAGE YETU HAPA