Friday 6 February 2015

SAKATA LA MREMA KUWA NA UKIMWI LATINGA BUNGENI, AMSHUSHIA SHUTUMA NZITO JAMES MBATIA


Mbunge wa Vunjo Dkt Augustine Mrema (TLP) ametoa shutuma zake bungeni Dodoma akimtuhumu mbunge wa kuteuliwa na rais James Mbatia kuwa amekuwa akimpakazia mambo mabaya kwa wapiga kura wa jimbo lake kuwa ana UKIMWI

Mrema amesema kuwa mbunge huyo amekuwa akipita jimboni kwa kwake na kusema kuwa wasimchague mbunge huyo kwa kuwa ana UKIMWI na hana maisha marefu hapa duniani

Ametoa kauli hiyo bungeni Dodoma na kusema "Napenda kusema kuwa mimi ni mbunge halali wa Vunjo na Mbatia hatapata jimbo hilo, na natangaza kuwa nitagombea tena na hafi mtu hapa"

Amesema ataendelea na shughuli zake jimboni mwake kama kawaida kwa kuwa yupo imara kiafya.
-EddyBlog.




0 comments:

Post a Comment

OFFICIAL MEMBER

OFFICIAL MEMBER

Please Share This Site

HABARI ZETU

LIKE PAGE YETU HAPA