Sunday, 8 March 2015

ANGALIA MAMBO MATANO YA KUFANYA MARA TU UNAPOKUTANA NA MPENZI WAKO BAADA YA KUACHANA MUDA MREFU

JUA TABIA ZA MSICHANA ANAYEPENDA LAKINI HAWEZI KUSEMA!!!

Dakika chache za kwanza tunapokutana na wapenzi wetu baada ya kuachana kwa kitambo kifupi zinaumuhimu sana.  Kitambo hiki ni kile ambacho labda mpenzi wako alikuwa kazini au safarini, umepita muda fulani hamjaonana, yamkini moyoni ulitamani kumwona au hata kule kuhisi kumkosa (kummiss) kulishaanza kupoa, jiulize mara utakapomwona, labda ni uwanja wa ndege, kituo cha basi, au amefungua mlango tu kuingia nyumbani.  Je unafanya nini?.  Kile utakaco kifanya hapa kina nafasi kubwa katika kuua taratibu penzi na ukaribu wenu (intimacy) au kulijenga kwa kasi kubwa. Ni uchaguzi wako, ingawa unashauriwa kufanya haya yafuatayo.

1.     Jiandae wewe mwenyewe kiakili
Kabla hamjaonana uso kwa uso andaa vema akili yako kumlaki mpenzi wako.  Fikiri mawazo mazuri na siyo yaliyo mabaya kumhusu yeye.  Usiwaze kumwagia lawama mara tu utakapomwona. Wengine mara tu wamwonapo mpenzi ameingia huanza kukurupuka kuuliza kama kaja na zawadi, na ole wake ukute kasahau huo moto utakao waka hapo! Panga nafsini mwako kitu au tukio la kufurahisha utakalomfanyia mara ukimwona.  Mara nyingine unaweza kumuuliza kwa simu muda atakapowasili ili uweze kujiandaa vile unavyodhani.

2.     Jiangalie muonekano wako
Dakika ya kwanza tu mnapotazamana yaweza kuathiri muendelezo mzima wa siku yenu.  Muonekano wako wa uso, tabasamu lako, harufu yako (nzuri au mbaya) vyaweza kumdaka au kumkimbiza mpenzi wako, haswa yule wa kiume.  wanaume pia nao wanachakufanya hapa, haupaswi kupokewa ukiwa rafurafu, mchafu, unatoa harufu mbaya ya mwili au ya viatu.  Jiangalie, nywele na ndevu zako zikoje, meno yako yanaonekanaje na hata ngozi yako hususani ya usoni. Mwonekano wako huzungumza zaidi vile unavyojiona wewe mwenyewe. Hauhitaji kusema mimi sijipendi, bali kuonekana kwako kutatoa ujumbe.  Jaribu uwezavyo kuwa mwenye mvuto mara mtakopokuwa na umpendaye.

3.     Onyesha tabasamu la pendo kwa mpenzi wako
Panga muda wako ili uweze kumsalimu mpenzi wako kwa tabasamu.  Acha mpenzi wako ajue kuwa yeye ni wa kipaumbele, na ni muhimu kwako, usimpokee kwa staili ya kumwonyesha humjali.  Tabasamu  linaweza kusema “I love you”  kuliko hata maneno au zawadi. Tabasamu halina gharama yoyote, ni la bure na lipo wakati wowote, kinachokushinda kulitumia ni nini?

Hata kama hujisikii kutabasamu, jitahidi kwa nama yoyote kuonyesha kuwa unaweza pia kutabasamu.  Jifanyishe pale mazingira yanapolazimu, hususani katika dakika nne za mwanzo. Ikiwa utajifanyisha vizuri, hisia njema zaweza kuibuka na  yale maumivu ya ndani ya moyo kutoweka taratibu.

4.     Salimianeni kwa kukumbatiana na kwa busu
Kuwa na mtu anayetusubiri mara tutakapofika sehemu au mara tutakapofungua mlango ni jambo ambalo wengi wetu tunalipenda,  kama kubusu sio mtindo au pendeleo lako basi tafuta njia nyingine ya miili yenu kugusana mara mnapoonana. Mfano kushikana mikono, kumshika mwenzako nywele au kichwa, nk. Mgusano wa mwili ni muhimu na unashauriwa kwa afya ya penzi lenu.

5.     Tengeneza mazingra mwanana
Jipeni muda wa kupumzika na kupumzisha akili kabla ya kuanza kuzungumzia matatizo yenu. Kila anayeingia nyumbani nakukuta anapokelewa na makelele na mikiki mikiki mara nyingi hutamani kuondoka.

Kila anayekuwa nyumbani kwanza kabla ya mwenzake anawajibika kutengeneza mazingira ya hisia nzuri, ingawa baada ya hapo wote wawili pia mnawajibu wa kuendeleza hisia hizi njema na  mazingira ya amani yaliyopo.

Wale ambao wanafanya kazi nje ya nyumbani huhitaji utulivu  kidogo mara wanaporudi ili kutuliza akili na hisia zao, wengine watataka dakika 15 wengine dakika 20, watataka kujinyoosha kidogo, au kusikiliza muziki fulani bila maongezi mengi, ingawa pia wapo  wanaotaka kucheza na watoto mara  wanapofika nyumbani. Chochote na kwa hali yoyote uipendayo, jaribu kujielezea, na mueleze mwenzako aelewe mtiririko wa hisia zako, hii itawasaidia sana.

CREDIT-chrismauki.com

0 comments:

Post a Comment

OFFICIAL MEMBER

OFFICIAL MEMBER

Please Share This Site

HABARI ZETU

LIKE PAGE YETU HAPA