Tuesday 3 March 2015

BI. JOYCE MUJURI AKANUSHA MADAI YA KUMROGA RAIS ROBERT MUGABE




Aliyekuwa Makamu wa Rais wa Zimbabwe Bi. Joyce Mujuri ameleza kuwa amepakaziwa madai ya uongo, kuwa yeye aliwasiliana na waganga wa kienyeji kutoka Nigeria kula njama za kumuua rais Robert Mugabe.

Rais Robert Mugabe alitoa madai hayo dhidi ya Bi. Mujuri wakati wa maadhimisho ya miaka 91 ya kuzaliwa kwake, siku ya jumamosi katika makazi yaliyopo Victoria Falls.

Kiongozi huyo aliwaambia wafuasi wake kuwa Bi. Mujuru ambaye alifukuzwa katika madaraka ya umakamu wa rais mwaka jana, kutoshiriki kumroga Rais Mugabe akiwa utupu na waganga wawili wa Nigeria.

Baada ya kufanya hivyo waganga hao wa Nigeria walimuambia Bi. Mujuri kuwa rais, mkewe pamoja na watu wake wa karibu watakufa ndani ya siku chache.

0 comments:

Post a Comment

OFFICIAL MEMBER

OFFICIAL MEMBER

Please Share This Site

HABARI ZETU

LIKE PAGE YETU HAPA