EXCLUSIVE: MFAHAMU MWANDISHI WA SIMULIZI YA TANGA RAHA, ANAYEKUJA KWA KASI KATIKA UANDISHI WA SIMULIZI
Tanga Raha,jina hili huenda likawa siyo geni katika pita
pita zako mpenzi msomaji,kisa kilichosisimua wengi na kujizolea umaarufu sana
kupitia mitandao ya kijamii hasa whatsp.NANI HUYU ALIYE MTUNZI WA KISA HIKI NA
VINGINE VINGI???
Eddzaria Gerson Msulwa mzaliwa wa Tanga katika hospitali ya
Bombo mnamo 17/03/1993 ambaye amepata nafasi ya kuzungumza na FUNGUKA LIVE na kufunguka mengi juu ya alipotoka ,alipo na kule aendako twende sambamba ,,,,
FL: Ni lini ulianza
harakati za uandishi?
Eddy: Nikiwa na miaka 10 kwanza nilianza sanaa ya uchoraji na taratibu nikahamia
kwenye uandishi ambapo nikiwa shule ya sekondari nilikuwa nikiandika hadithi
fupi katika karatasi na kuwapa rafiki zangu wasome na hapo wakaanza kunipa moyo kuwa nina
kipaji.
FL: Uliwezaje kugawa muda wa masomo hasa ya sekondari pamoja
na kazi ya kuandika?
Eddy: Ukweli nilikuwa naiba muda wa “prep”,wakati wenzangu
wanasoma mimi nilikuwa nikandika lakini kwa wakati Fulani nilizingatia masomo
kiasi cha kuweza kufaulu kujiunga na elimu ya kidato cha tano na sita ambapo
kwa bahati mbaya nilipata majanga nikashindwa kuhitimu kidato cha sita.
FL: Je huo ndio ulikuwa mwisho wa safari yako ya elimu?
Eddy : Hapana,japokuwa nilipoteza dira kiasi cha kushindwa
kuendelea kuandika kwa kipindi hicho,mama alinishauri nisomee masuala ya afya
na kwa kuwa haikuwa dhamiri yangu pia nilishindwa kuhitimu masomo katika chuo
hicho,hapo nikahama na kujiunga na kikundi cha sanaa mwaka 2012 na kushiriki
katika tamthilia iliyoitwa Tanganyika ambapo pia sikuweza kudumu kwani haikuwa
sehemu niliyopangiwa na mwenyezi Mungu.
FL: Wapi ulielekea baada ya kutoka kwenye sanaa ya maigizo?
Na je muda wote huu wa mahangaiko familia yako ilikuwa inakuchukuliaje?
Eddy: Kwanza kabisa familia yangu ilikuwa nami bega kwa bega
ukizingatia baba yangu (marehemu Gerson) ndiye aliyenivutia na kunihamasisha
kuchipua kipaji changu cha uandishi,vile vile mama yangu alihitaji kuona
nafanikiwa kwa kile kitu ambacho ningekifanya kwa “amani ya moyo”.
Vile vile ni mwaka huo huo wa 2012 ndipo nilipoanza harakati
za uandishi katika mtandao wa kijamii wa Facebook ambapo nilikuwa napost story
kwenye “magroup” na kwenye kurasa yangu binafsi lakini mwitikio haukuwa mzuri
kabisa,ila kwa bahati nzuri nilipata nafasi ya
kuelekea Nairobi na kupata mafunzo ya sanaa ya uandishi kwa mwaka mmoja.
Niliporejea mwishoni mwa mwaka 2013 niliendelea kuandika
hadithi Facebook na kwa mara ya kwanza niliweza kupata *LIKES 10* kwangu
yalikuwa mafanikio makubwa sana.
FL: Hadi sasa tofauti na TANGA RAHA ni story gani ambayo
umeandika na inafanya vizuri??
Eddy : Hadi sasa nimefanikiwa kuandika simulizi nyingi
ikiwemo TANGA RAHA,MY MOMS FRIEND,SORRY MADAM,SEX DEALERS ,PRESIDENTS WIFE na
nyinginezo.
FL: Ni njia gani unayotumia kusambaza simulizi zako na kuepuka
wizi ambao ndiyo changamoto kubwa?
Eddy : Kwasasa namiliki Official Page yangu Facebook
inayoitwa Simulizi Za Eddy ambayo ina Likes takribani 20 elfu na hapo ndipo kwa
wingi napost simulizi zangu,vile vile nazisambaza kupitia whatsp ambapo mdau
anachangia kiasi kidogo kwa ajili ya “kusapoti” juhudi yangu.
Kwa suala la kukabiliana na wizi nimeanza kusajili simulizi
ninazopost hivyo kuwa mmiliki halali kisheria.
FL: Wadau wengi wamezoea kusoma simulizi nyingi kupitia
vitabu,vipi umejipangaje katika hilo au ndiyo umeamua kuwa msimulizi katika
mitandao?
Eddy : Hapana,nimejipanga kutoa vitabu,ila masuala ya uchumi
yalikuwa kikwazo pia familia ilipita katika wakati mgumu wa kumuuguza baba
ambaye alifariki Februari mwaka Huu…….
FL: Asilimia kubwa ya simulizi zako zinahusisha hisia za
mapenzi na mambo flani ya kikubwa (+18) ,kwanini?
Eddy: Hahaha..,ni kweli lakini
pia nachanganya maudhui ,lengo kuu ni kuelimisha jamii katika Nyanja zote za
maisha japo mapenzi yagusa karibu Nyanja zote.
FL: Nashukuru sana kwa Kuitika
wito wa FL, msomaji akiwa amevutiwa na simulizi zako je atakupataje.
Eddy : Kwa akayehitaji simulizi
za Eddy awasiliane name kwa simu namba 0657 072 588.
0 comments:
Post a Comment