MAREHEMU JOHN KOMBA AACHA MKE WA NA WATOTO 11....!!!!
08:00 |
No Comments |
Mbunge wa Mbinga Magharibi na Mkurugenzi wa Kikundi cha Tanzania One Theatre (TOT) Kapteni John Komba amefariki dunia jana alipokuwa akipelekwa katika hospitali ya TMJ jijini Dar es Salaam baada ya kuzidiwa.
Taarifa za kifo hicho zimethibitishwa na Hospitali ya TMJ, ofisi ya Bunge na Chama Cha Mapinduzi na kwamba kwa sasa taratibu za maziko yake zinaendelea kufanywa .


Aidha taarifa za hivi punde kutoka nyumbani kwake maeneo ya Mbezi Beach Tangi Bovu zinaeleza kuwa maelfu ya watu kutoka katika kada mbalimbali wanaendelea kumiminika nyumbani kwa marehemu ili kutoa faraja kwa familia kwani marehemu ameacha mjane mmoja na watoto kumi na moja.
Akizungumza na tovuti hii mmoja wa madaktari aliyempokea wakati anafikishwa hospitali ya TMJ, Dk Elisha Ishan amesema Komba alifikishwa hospitalini hapo saa 10 jioni jana akiwa mahututi .

"Nilimpokea nilianza moja kwa moja kumpima shinikizo la damu na vipimo vingine lakini tayari vilikuwa havifanyi kazi na hapo ndipo tukathibitisha kuwa ndugu yetu ameaga dunia," amesema Dk Ishan
Pamoja na hayo Dk Ishan amekwepa kutaja moja kwa moja chanzo cha kifo cha marehemu, hata hivyo amesea Kapteni Komba alikuwa na tatizo la shinikizo la damu na kwamba siku za karibuni alifika hospitalini hapo kwenye kiliniki yake ya shinikizo la damu.
Marehemu Kaptain Komba alizaliwa Marchi 18 mwaka 1945 alipata elimu ya msingi huko nchini Tanzania katika shule ya Lituhi baadae elimu ya sekondari katika shule ya sekondari ya Songea iliyopo kusini mwa Tanzania kuanzia 1971 hadi mwaka 1974.
Mwaka 1975 hadi mwaka 1976 Marehemu John Komba alijiunga na chuo cha ualimu kilichopo Kleruu Iringa, Kusini Magharibi mwa Tanzania ambapo alihitimu cheti cha ualimu.
Marehemu John Komba ni mwanajeshi ambaye alipata mafunzo ya uafisa wa Jeshi katika chuo cha Maafisa wa Jeshi kilichopo Monduli kaskazini mwa Tanzania mwaka 1978 hadi mwaka 1978.
Keptain John Komba pia alipata mafunzo mengine ya siasa kutoka chuo Kikuu cha Washngton International ambapo alitunukiwa shahada ya siasa mwaka 2006 hadi mwaka 2008.
Related Posts:
BREAKING NEWZ; MWIMBAJI MWINGINE WA MUZIKI WA INJILI NCHINI AFARIKI DUNIA Zikiwa ni takribani wiki tatu tangu tasnia ya muziki wa injili nchini kumpoteza mmoja wa waimbaji wake marehemu mchungaji Debora Saidi, taarifa am… Read More
SOMA HII STORY HUYU DADA ALIYEKUTANA NA MWIGIZAJI SHAMSA FORD LEO. Kupitia ukurasa wa mtandao mmoja wa kijamii leo hii, mwanadada mwigizaji Shamsa Ford amepost ujumbe huu kwa wale wadada wote wanopenda k… Read More
EXCLUSIVE ::PROFESSOR JAY AMEANZA KU SHOOT VIDEO YA WIMBO KIPI SIJASIKIA,,,CHEKI PICHA Professor Jay akiwa na pingu mkononi na P-Funk akiwa kwenye vazi la hakimuKatika picha ambazo zimetoka hivi punde zimemuonyesha prodyuza mko… Read More
AUNT EZEKIEL AFUNGUKA::ASEMA HANA GUNDU NA MIDUME,,CHEKI HAPA Baada ya kudaiwa kuwa na gundu kufuatia kila mwanaume anayeishi naye kuandamwa na majanga, staa wa Bongo Movies, Aunt Ezekiel Grayson ameib… Read More
DAYNA NYANGE AFUNGUKA ,AELEZEA CHANGAMOTO ANAZOPATA BAADA YA KUJICHUBUA Mwimbaji wa kike Dayna Nyange azungumzia jinsi alivyokutana na changamoto nyingi baada ya kuamua kubadili rangi ngozi yake na kuwa nyeupe. … Read More
0 comments:
Post a Comment