Tuesday, 3 March 2015

WATETEZI WA HAKI ZA WANYAMA CHINA WAPINGA TAMASHA LA WALA NYAMA YA MBWA


Tamasha la kila mwaka la nyama za mbwa linalofanyika Yulin, Guizhou nchini China kusherehekea majira ya joto limeibua mjadala mkali baina ya watetezi wa haki za wanyama na jamii inayokula nyama ya mbwa.

Nyama ya mbwa kwa asili huchukuliwa kama mlo mtamu katika baadhi ya maeneo ya China yakiwemo ya Mkoa wa Kusini wa China wa Guizho ambapo tamasha hilo limekuwa likifanyika kila mwaka kwa zaidi ya miaka 100 iliyopita.

Watetezi wa haki za wanyama wamesema nyama ya mbwa imekuwa ni sehemu ya milo ya kila siku nchini China ambapo inakisiwa mbwa alfu 10 huchinjwa na kuliwa katika siku ya tamasha hilo pekee, ambapo nyama ya mbwa huuzwa kiasi cha dola 6 kwa kilo moja.

0 comments:

Post a Comment

OFFICIAL MEMBER

OFFICIAL MEMBER

Please Share This Site

HABARI ZETU

LIKE PAGE YETU HAPA