Sunday, 26 April 2015

LIGI KUU NCHINI UINGEREZA, MANCHESTER CITY YAITANDIKA ASTON VILLA 3-2

Mabao kutoka kwa Sergio Aguero, Aleksandar Kolarov na Fernandinho yalitosha kuwapa ushindi wa magoli 3-2 timu ya soka ya Manchester City katika mchezo wa ligi kuu nchini Uingereza dhidi ya Aston Villa jana. 

Wakicheza katika uwanja wao wa nyumbani wa Etihad, Manchester City iliwachukua dakika tatu za kwanza kuandika bao la kwanza kupitia kwa Aguero. 

Kwa ushindi huo, mabingwa hao watetezi ambao hata hivyo nafasi yao ya kuutetea ubingwa msimu huu imepotea, wamefikisha pointi 67 nyuma ya vinara wa ligi hiyo Chelsea wenye pointi 76.

Mabao ya Aston Villa yaliwekwa kimiani na wachezaji Cleverley, Sanchez 

Kocha wa Aston Villa Tim Sherwood ( kushoto ) akitoa maelekezo kwa wachezaji wake.


Sambamba na hili yafuatayo ni matokeo ya timu nyingine pamoja na msimamo wa ligi hiyo kabla ya mechi za leo jumapili.


0 comments:

Post a Comment

OFFICIAL MEMBER

OFFICIAL MEMBER

Please Share This Site

HABARI ZETU

LIKE PAGE YETU HAPA