Sunday, 19 April 2015

YANGA YABANWA MBAVU NYUMBANI NA WAARABU CHEKI PICHA


Timu ya Yanga imelazimishwa sare ya bao 1-1 na Etoile du Sahel ya Tunisia katika mchezo wa kwanza wa raundi ya 16 bora ya kombe ya shirikisho barani Afrika uliomalizika hivi punde katika dimba la taifa Dar es salaam.




Yanga wamekuwa wa kwanza kupata bao kupitia kwa nahodha Nadir Haroub ‘Canavaro’ kwa mkwaju wa penalti baada ya Simon Msuva kuangushwa katika eneo la hatari na Etoile wakasawazisha dakika ya 46.
Katika mchezo wa leo Etoile wameonekana kuwa wazuri kuliko Yanga, ingawa safu ya ulinzi ya Yanga ikiongozwa na golikipa Ally Mustapha imeonesha umahiri wa kuokoa hatari nyingi kutoka kwa timu hiyo ya Tunisia.





Mechi ya marudiano itafanyika wiki mbili zijazo nchini Tunisia na Yanga itahitaji ushindi wowote au sare ya kuanzia mabao 2-2.

0 comments:

Post a Comment

OFFICIAL MEMBER

OFFICIAL MEMBER

Please Share This Site

HABARI ZETU

LIKE PAGE YETU HAPA