CHEKI MAAJABU:TEMBO WAFUNGA BARABARA KUMSAIDIA MWENZAO ALIYEDONDOKA
16:59 | No Comments |
Tembo wakiwa wamemzunguka mwenzao kumpatia msaada.
SUALA la umoja si kwa wanadamu pekee bali hata wanyama kama tembo nao wanao umoja miongoni mwao.
Katika tukio lililonaswa kwenye video huko nchini Afrika Kusini na kuwekwa kwenye mtandao wa Youtube linawaonyesha tembo walioamua kufunga barabara na kusababisha foleni ya magari ili wamuokoe mwenzao aliyedondoka katikati ya barabara hiyo.
Tembo huyo akiwa chini baada ya kudondoka.
Tembo huyo mdogo alidondoka wakati akitembea barabarani kwenye Hifadhi ya Taifa ya Kruger iliyopo Afrika Kusini.
Baada ya tukio hilo tembo wakubwa walikuja na kufunga barabara ili kumpatia msaada mwenzao huyo.
Tembo huyo akijaribu kuinuka kwa msaada wa wenzake.
Baada ya kuangaika kwa muda, tembo huyo mdogo alifanikiwa kusimama kwa msaada wa wenzake na kuendelea na safari ambapo wenzake nao waliamua kutoka barabarani na kuwafanya madereva wa magari kuendelea na safari zao.
...Hatimaye tembo huyo akafanikiwa kuinuka.
...Akitokomea na wenzake.
0 comments:
Post a Comment