Saturday 16 May 2015

KAMA UNAHITAJI MPENZI BORA,JIEPUSHE NA WANAWAKE WA AINA HII

Image result for black sexy woman
Hakikisha unawakwepa aina hii ya wanawake ili usijiingize kwenye matatizo. Nitakwambia ni kwa nini…..
1.Demu wako wa zamani
Ni vizuri kutorudia mahusiano ya zamani na zaidi kama kwenye mahusiano yenu ya mwanzo mambo hayakuishia kwa uzuri. Sababu kuu ya msingi, kiukweli ni kwamba hakika mwanzoni mlikuwa hamuendani na ndio sababu ya iliyopelekea kuvunjika kwa mahusiano yenu, ndani ya hizo sababu kuna vitu vilivyopolekea kutokea kwa hayo, ukichunguza na kuziangalia kwa makini utagundua ni za asili na ambazo si rahisi kwa mmoja wenu kuzibadilisha sababu ni vitu au mambo ambayo yatakuwa ni ya damuni.

2.Dada wa rafiki yako kipenzi
Epukana na kujiingiza kwenye mahusiano na dada wa rafiki yako. Si tu kwamba utaweza kujiingiza kwenye uhasama na chuki kama mambo hayatakwenda sawa, ila pia utaweza kujiweka kwenye mazingira ya kujikuta siku moja unapigwa hata ngumi za uso sababu tu ulimuumiza dada yake. Pia, utaweza kumkosa mtu ambaye ndie alikuwa ni kimbilio lako kwa mambo mbalimbali pale ambapo itatokea wewe na dada yake mambo kutokwenda sawa, sababu hapo patakuwa na mgongano wa kimaslahi kwa huyo rafiki yako.

3.Wanawake wenye mambo mengi
Kiukweli, kutoka na watu kama hawa kinaweza kuwa ni kitu cha kufurahisha, ila mwisho wa siku itakuingiza kwenye matatizo. Mara zote kumbuka ni vyema kuwa salama kuliko kujuta. Usijiingize kwenye majaribu ambayo utakuja kuyajutia kwa maisha yako yote.

4.Wanawake wanaopenda hela kupitiliza (Wachunaji)
Kuwa mbali nao, labda kama unataka salio lako limalizike pasipo wewe kujifahamu. Naamini hili kila mmoja analifahamu na halihitaji darasa zaidi.


Image result for black sexy woman
5.Demu wa zamani wa rafiki yako
Kama unathamini urafiki wako na mshikaji wako achana na habari ya kutoka na aliyekuwa demu wake. Mambo yanaweza kubadilika na kuwa kama au zaidi ya yaliyotokea kwa rafiki yako na ikaja kula kwako zaidi. Wakati mwengine inaweza tengeneza chuki kati yako na rafiki yako, huku akiamini kwamba ulikuwa unatoka au kumnyemelea demu wake toka zamani.Vile vile kumbuka kuwa mahusiano yanahitaji uhuru,JE UTAKUWA HURU KUJUMUIKA NA RAFIKI YAKO HUKU FIKA UKUJUA KUWA ULIENAE SASA ALIKUWA WAKE?

Lakini je utaweza kuwa na uhuru uliokuwa nao kwa rafiki yako kama ilivyokuwa zamani.

SIKATAI MAPENZI NI HISIA,,,ILA NIKUKUMBUSHE KUWA KUNA MAISHA BAADA YA MAPENZI ngoja nisisitize kwa kizungu THERE IS LIFE BEYOND ROMANTIC RELATIONSHIP.

Hata hivyo nikukumbushe kuwa unaweza ukawa na miongoni mwa niliyoyataja hapo juu,usifadhaike,jipime kama kweli upo huru na unapata kile ulichokilenga kabla ya kuanza mahusiano.Kama kila kitu kipo sawa WISH YOU ALL THE BEST,na usisahau kumshirikisha Mungu (kwa imani yako) kwani bila yeye mimi na wewe sii lolote.
-KD MULA

0 comments:

Post a Comment

OFFICIAL MEMBER

OFFICIAL MEMBER

Please Share This Site

HABARI ZETU

LIKE PAGE YETU HAPA