Saturday 16 May 2015

TUME YA MIPANGO YATEMBELEA EPZA






Displaying DSC_5719.JPG
Meneja wa Utekelezaji na Maendeleo wa Mamlaka ya Ukanda Maalumu wa Uwekezaji nchini (EPZA), Mhandisi Keneth Haule (Kulia) akiukaribisha ugeni kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango walipokwenda kujionea maendeleo ya miradi ya kimkakati inayotekelezwa katika Mamlaka, Mabibo jijini Dar es Salaam. Katikati ni Kiongozi wa Msafara huo, Bibi Florence Mwanri. Wengine pichani ni Bw. Abel Shirima (Kushoto), Bw. Aloyce Andrea (Wapili Kushoto), na Bw. Omary Abdallah (Wapili Kulia).



Displaying DSC_5720.JPG
Kiongozi wa Msafara kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango, Bibi Florence Mwanri (Kushoto) akizungumza na Mkurugenzi wa Mipango wa EPZA, Bw. Lamau Mpolo (Katikati) wakati walipotembelea kujionea maendeleo ya miradi ya kimkakati inayotekelezwa na Mamlaka hiyo jijini Dar es Salaam. Anayewasikilizia ni Meneja wa Utekelezaji na Maendeleo wa Mamlaka, Mhandisi Keneth Haule (Kulia).
Displaying DSC_5722.JPG
Mkurugenzi wa Mipango wa EPZA, Bw. Lamau Mpolo (Katikati) akizungumza na Kiongozi wa Msafara kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango, Bibi Florence Mwanri (Kushoto) wakati Bibi Mwanri na ugeni wake walipotembelea Ofisi za Mamlaka kujionea maendeleo ya miradi ya kimkakati inayotekelezwa katika Mamlaka, Mabibo jijini Dar es Salaam. Anayewasikilizia ni Meneja wa Utekelezaji na Maendeleo wa Mamlaka, Mhandisi Keneth Haule (Kulia).
Displaying DSC_5728.JPG
Bibi Lilian Kalengo (Kulia), muwakilishi wa Kiwanda cha Tooku Garments akiwaonesha suruali ya jeans wageni kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango walipokwenda kujionea maendeleo ya miradi ya kimkakati inayotekelezwa eneo la Mamlaka ya Ukanda Maalumu wa Uwekezaji nchini (EPZA), Mabibo jijini Dar es Salaam. Kiwanda hicho ni moja ya viwanda 12 vilivyoanza uzalishaji katika Ukanda wa huo.



Displaying DSC_5729.JPG
Kiongozi wa Msafara kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango, Bibi Florence Mwanri (Kushoto) akiangalia moja ya suruali zinazotengezwa na kiwanda cha Tooku Garments kilichopo katika eneo la Mamlaka ya Ukanda Maalumu wa Uwekezaji nchini (EPZA), Mabibo jijini Dar es Salaam.Displaying DSC_5731.JPG
Mmoja wa mabinti wa Kitanzania walioajiriwa na Tooku Garments akiwa kazini.
Displaying DSC_5733.JPG
Wakina dada wakiendelea na kazi ya utengenezaji wa suruali za jeans zinazotengenezwa na kiwanda cha Tooku Garments kilichopo katika eneo la Mamlaka ya Ukanda Maalumu wa Uwekezaji nchini (EPZA), Mabibo jijini Dar es Salaam.Displaying DSC_5780.JPG

Displaying DSC_5776.JPG


Mandhari ya kuvutia ya Mamlaka ya Ukanda Maalumu wa Uwekezaji nchini (EPZA) yaliyopo Mabibo, jijini Dar es Salaam.

PICHA NA SAIDI MKABAKULI

0 comments:

Post a Comment

OFFICIAL MEMBER

OFFICIAL MEMBER

Please Share This Site

HABARI ZETU

LIKE PAGE YETU HAPA