Sunday 17 May 2015

RAIS PIERRE NKURUNZIZA AHUTUBIA UMMA HADHARANI TANGU JARIBIO LA MAPINDUZI


Rais wa Burundi Pierre Nkurunziza amesema nchi yake inakabiliwa na tishio la shambulio la kigaidi kutoka kundi la al-Shabaab la nchini Somalia.

Rais Nkurunziza ametoa kauli hiyo wakati akiongea hadharani kwa mara ya kwanza mbele ya umma tangu kushindwa kwa jaribio la kumpindua jumatano ya wiki iliyopita.

Katika hotuba hiyo Nkurunziza hakuzungumzia lolote kuhusu jaribio hilo la mapinduzi, ambalo limetokea baada ya wiki kadhaa za machafuko ya kumpinga asiwanie tena urais.

Siku ya jumamosi watu 18, walifikishwa mahakamani na kufunguliwa mashtaka ya kusaidia mapinduzi.

0 comments:

Post a Comment

OFFICIAL MEMBER

OFFICIAL MEMBER

Please Share This Site

HABARI ZETU

LIKE PAGE YETU HAPA