Sunday 21 June 2015

HUYU NDIYO MTANGAZA NIA ANAEWANIA KUMNG'OA LEMA UBUNGE ARUSHA MJINI

Mkurugenzi mtendaji wa kampuni ya Bushbucks Safaris iliyopo jijini Arusha Mustafa Panju akiongea na vyombo mbalimbali vya habari ofisini kwake ,akitangaza rasmi kuwania kiti cha ubunge jimbo la Arusha mjini kupitia tiketi ya chama cha mapinduzi CCM
Mkurugenzi mtendaji wa kampuni ya Bushbucks Safaris iliyopo jijini Arusha Mustafa Panju akiongea na vyombo mbalimbali vya habari ofisini kwake ,akitangaza rasmi kuwania kiti cha ubunge jimbo la Arusha mjini kupitia tiketi ya chama cha mapinduzi CCM kushoto ni mke wake
Kassim Mamboleo ambaye ni katibu wa kamati ya ushindi ya mgombea Mustafa Panju akitoa utambulisho kwa vyombo vya habari Taswira katika mkutano huo na waandishi wa habari
Na Pamela Mollel, Arusha
JIMBO la Arusha ni moja ya jimbo ambalo linaonekana kuwa ni jimbo lenye siasa komavu, kutokana na hali hiyo limeonekana kuongoza kwa vurugu na uvunjifu wa amani , ambapo kupitia kwa Mtangaza nia wa ubunge jimbo la Arusha mjini Mustafa Panju amewahakikishia wananchi kurudisha amani hiyo.
Jimbo hilo ambalo linashikiliwa na Mbunge wa Arusha mjini kupitia chadema ,Godbless Lema ambaye hivi sasa ametangaza tena kulitaka jimbo , ambapo hadi hivi sasa jumla ya wagombea 18 kupitia chama chamapinduzi wamejitokeza kumg’oa mbunge huyo.
Akizungumza na waandishi wa habari jana wakati akitangaza nia ya kuwania ubunge kupitia chama cha mapinduzi , Panju alisema kuwa ipo sababu ya kurudisha jimbo hilo mikononi mwa CCM kwa kuwa CCM ni chama kinachopenda amani na kinachodumisha amani.
‘kila mmoja anatambua jinsi ambavyo jiji la Arusha hivi sasa halina amani kabisa na hakuna mtu anayedhubutu hata kutembea usiku , ila nitahakikisha linakuwa jiji la amani na utulivu na kuwawezesha wananchi wake kufanya shughuli zao bila hofu yoyote’alisema Panju.
Alifafanua zaidi kuwa,mbali na kurejesha amani jijini Arusha atahakikisha anaondoa makundi mbalimbali yaliyopo miongoni mwa wananchi kwa kuwafanya wawe wamoja na wenye ushirikiano ili kuleta mabadiliko katika jimbo la Arusha kwa ujumla.
Pia alisema kuwa,wagombea wote wa nafasi ya ubunge katika chama ni
wajibu wao kujenga Undugu,Upendo, na urafiki wakati wote ili kuepuka kujenga makundi ndani ya chama kwa misingi mbalimbali ya ukabila, udini na hata urangi.
Panju alisema kuwa, swala la kuwepo kwa makundi na vikundi katika vyama na kwa wananchi linapaswa kuangaliwa kwa umakini kwani likiendelea kuwepo linajenga uhasama ndani ya chama na pia uhasama unaoleta ubaguzi ndani ya nchi kwa ujumla.

0 comments:

Post a Comment

OFFICIAL MEMBER

OFFICIAL MEMBER

Please Share This Site

HABARI ZETU

LIKE PAGE YETU HAPA