Saturday 11 July 2015

LOWASSA, PINDA WAENGULIWA RASMI TANO BORA CCM ,MEMBE,MAGUFULI WAPETA




Ni wazi sasa kuwa kitendawili kilichokuwa kikisubiria kuteguliwa na wengi kuhusu nani ataingia tano bora katika mbio za kuwania urais kuptia chama cha Mapinduzi CCM kimeteguliwa kwa chama hicho kuyadhihirisha majina matano mbele ya umma wa Tanzania ambapo taarifa rasmi zinasema
"Kikao cha KAMATI KUU (CC) kimekamilika na kufanikiwa kuwateua wagombea wake 5 ambao ni: 

1) Bernard Membe 2) John Magufuli 3) Asha Rose Migiro 4) January Makamba 5) Amina S. Ali.

 Hatua inayofuata ni majina ya wagombea hawa kukabidhiwa kwa HALMASHAURI KUU YA TAIFA (NEC) ili kupata majina matatu (3) yatakayopigiwa kura kwenye Mkutano Mkuu asubuhi  "


Alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari muda mfupi uliopita katibu mwenezi wa CCM Nape Nnauye amethibitisha kuwa taarifa zilizosambaa awali kupitia mitandao kuwa ni sahihi na sasa chama kinajiandaa na mikutano inayofuata.

Nape pia aligusia suala la baadhi ya wajumbe wa kamati kuu kutamka hadharani kuwa hawajaridhishwa na maamuzi hayo na kusema chama kitalishughulikia hilo na kukanusha kuwa ndani ya chama hakuna mpasuko.

Image result for lowassa
PICHA NA MAKTABA

Kufuatia kutajwa kwa majina hayo ni wazi kuwa masikio ya walio wengi ni kwa aliyekuwa waziri mkuu wa Tanzania Mh Edward Lowassa atafanya nini hasa baada ya kutumia nguvu kubwa kuzunguka nchi nzima kusaka wadhamini lukuki na aliyeonekana kupendwa na walio wengi.

Vile vile sasa UKAWA wanasubiriwa ili kuona nao wartamteua nani hasa ikisemekana walikuwa wakisubiri CCM ipitishe mgombea wake ambaye atapatikana ndani ya saa 24 kuanzia sasa.

FUNGUKA LIVE ITAENDELEA KUKUJUZA NINI KINAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

OFFICIAL MEMBER

OFFICIAL MEMBER

Please Share This Site

HABARI ZETU

LIKE PAGE YETU HAPA