Sunday 12 July 2015

MTANZANIA MWINGINE AFANYA MAJARIBIO UJERUMANI, ALIKUWA STAND UNITED

MISHETTO (WA TATU KULIA) AKIWA KATIKA MAJARIBIO.
Mtanzania mwingine ambaye alikuwa anakipiga katika kikosi cha Stand United, sasa anapambana kupata timu nchini Ujerumani.


Charles Mishetto ameishaanza majaribio katika kikosi cha Rapid BSC.

Mishetto amezungumza na SALEHJEMBE kutoka Ujerumani na kutoa maelekezo haya.
 
MISHETTO (WA PILI KULIA)
“Tanzania nilikuwa nakipiga Stand United na hapa nitachezea katika timu ya ligi dalaja la tano eneo la Sachsen wes.

“Timu inaitwa Rapid bsc Chemnitz, ingawa kwenye mazoez kuna viongozi wa timu nyingine kubwa wameonesha nia ya kunisajili.
 
....WA TATU KULIA.
Lakini kwa sasa niko hapa inawetekana kabisa nikasajiliwa na timu hii ama hiyo timu nyingine wananifuatilia na wamependa kipaji changu na aina ya African Culture Football.

“Msimu uliopita niliwahi kuchezea ligi daraja la nne kule Munich kabla sijarud Tanzania na kusajiliwa na Stand united.
“Mawakala wengi waliniona na timu nyingi zilikua zikiwasilaina na mimi ila sasa nimepata hapa na niko kwenye trial nina week sasa na kufikia week inayokuja nitakufahamisha nimesaini wapi na contract ya muda gani.”


KILA LA KHERI MISHETTO.
-salehejembe

0 comments:

Post a Comment

OFFICIAL MEMBER

OFFICIAL MEMBER

Please Share This Site

HABARI ZETU

LIKE PAGE YETU HAPA