Sunday, 30 August 2015

DANCE 100% 2015 NUSU FAINALI YAFUNIKA OYSTERBAY





             Kundi la 'Majoker Crew' wakiingia stejini kwa namna ya pekee kabisaa.


Majaji wakiendelea na shughuli yao ya kupima uwezo kukokotoa na kutoa alama kwa madansa.


                             Kundi la 'The Winners Crew' wakionyesha makali yao kwa steji.



                                                          Mashabiki wakifuatilia mashindano kwa makini.



Mashindano ya Dance 100% 2015 hatua ya Robo Fainali hatimae yamekamilika na kufanikisha kupatikana kwa makundi 10 ambayo yanasonga mbele kulekea hatua ya fainali ya mashindano hayo makubwa Afrika Mashariki.



Kutokana na uwezo mkubwa walioonyesha mbele ya majaji Majokery, Wazawa Crew, The Best, Cute Babies, Best Boys Kaka Zao, The Winners, Team ya Shamba, The WD, Team Makorokocho na Quality Boys ndio makundi yaliyofanikiwa kuingia nusu fainali.



Upekee na mvuto wa aina yake kutoka kwa mashabiki kati ya mambo mengine ulikuwa ni muonekano mpya ya set ya Jukwaa la madansa jipya kabisa ambalo lipo juu lililowezesha kila aliyeweza kufika kujionea burudani ya dansi na ubunifu katika hali ya kipekee.




Kwa kipekee pia na kwa tathmini ya majaji, Kundi la Majokery ni kati ya washindano waliomwagiwa sifa nyingi kwa kuzingatia kuhusisha nyimbo za kitamaduni katika dansi yao, na vilevile usimuliaji wa hadithi kupitia kile walichokicheza.



Kama sehemu ya Tathmini ya mashindano hayo, Mratibu wa mashindano kutoka BASATA, Kwerugira Maregesi ametoa wito kwa makundi yaliyofanikiwa kuingia nusu fainali kuongeza mazoezi zaidi na kuzingatia vigezo vya mashindano kama siri pekee ya kuweza kushinda.



Mpango huo mzima ambao ulisimamiwa vizuri na majaji Super Nyamwela, Queen Darleen na Shetta na kushereheshwa na T Bway pamoja na Maggie Vampire, umeletwa kwako na team nzima ya East Africa Radio na East Africa TV na kudhaminiwa kwa nguvu kabisa na Coca Cola na Vodacom Tanzania.

0 comments:

Post a Comment

OFFICIAL MEMBER

OFFICIAL MEMBER

Please Share This Site

HABARI ZETU

LIKE PAGE YETU HAPA