Tuesday 18 August 2015

MABASI YA MWENDO WA HARAKA JIJINI DAR YAZINDULIWA RASMI

...Akikata utepe kama ishara ya uzinduzi huo.
 
...Akiwa tayari amepanda gari la mwendo wa haraka baada ya uzinduzi.
Mgeni rasmi, Hawa Ghasia, akizungumza jambo.
Mstahiki Meya wa Mkoa wa Dar es Salaam, Dkt.  Didas Massaburi (kushoto), akisalimiana na Sadick Mecky Said kabla ya uzinduzi.(P.T)

Gari la mwendo wa haraka likiwa limepaki sehemu ya uzinduzi huo.
Moja ya magari ya mwendo wa haraka ambalo ni fupi.
Baadhi ya wananchi wakitamani kuyaona magari hayo
Baadhi ya wafanyakzi wa DART na wananchi wakisikiliza taaarifa iliyokuwa ikisomwa kwa mgeni rasmi kabla ya uzinduzi.
Madereva wa Kichina waliokuja kwa ajili ya kutoa mafunzo ya udereva wa magari hayo ya mwendo wa haraka.
Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Kipolisi Dar es Salaam, Suleiman Kova (kushoto) akiwa na Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani, Mohammed Mpinga.
Baadhi ya wananchi waliokuwepo kwenye uzinduzi huo.
Mwonekano wa ndani moja ya magari hayo.
Baadhi ya wakazi wa eneo la Kimara wakiyashudia magari hayo yalipotua kituoni hapo.
Hawa Ghasia akishuka kwenye moja ya magari hayo mara baada ya kumaliza safari ya kutokea Ubungo-Kimara.
Baadhi ya wananchi waliopata fursa ya kuyapanda magari hayo kutokea Kimara wakiteremka kituo cha Ubungo.
Viongozi walioshiriki uzinduzi huo wakiwa katika picha ya pamoja baada ya kushuka katika moja ya magari hayo.
MABASI ya mwendo wa haraka jijini Dar es Salaam yamezinduliwa rasmi na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Hawa Ghasia, akiambatana na viongozi mbalimbali akiwemo Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Sadick Mecky Said.
Uzinduzi huo wa huduma ya mpito (interim service) umefanyika leo katika kituo cha DART kilichopo nje ya kituo kikuu cha mabasi yaendayo mikoani Ubungo.
Akizungumza na wananchi na wanahabari waliohudhuria hafla hiyo, Hawa Ghasia alisema kuwa jiji la Dar es Salaam ni la pili katika kutekeleza mradi huo baada ya Afrika ya Kusini.
Alisema kuwa wananchi wapokee huduma hiyo mpya ya usafiri kutokana hali halisi ya kwenda na wakati tofauti na kuendelea kutumia huduma ambazo haziko kiteknolojia zaidi.
Naye Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Sadick Mecky Said, akizungumza katika hafla hiyo amesema huduma hiyo itawawezesha wananchi kupunguza idadi ya magari yanayopita barabarani kwa wingi kwa kupanda gari moja tu la DART ambalo litakuwa ni kubwa lenye kutoa usafiri wa haraka.
Aidha amewataka wananchi kuwa makini wakati wanapokuwa barabarani hasa zile ambazo zitakazokuwa zikitumika kwa magari hayo ya mwendo wa haraka, akisema wananchi yeyote atakayepita katikati ya barabara hizo na kusababisha ajari atachukuliwa hatua kali hata kama gari la mwendo wa haraka litamgonga, kwani yeye ndiye atakayeonekana mwenye makosa kama ambavyo treni linapogonga mtu au gari.
“Mwananchi yeyote atakayepita katikati ya barabara hizi na kusababisha ajali atachukuliwa hatua kali mara moja na hata kama gari la mwendo wa haraka litamgonga, yeye ndiye atakayeonekana mwenye makosa huku akifananisha na barabara ya treni.”
(NA DENIS MTIMA/GPL)

0 comments:

Post a Comment

OFFICIAL MEMBER

OFFICIAL MEMBER

Please Share This Site

HABARI ZETU

LIKE PAGE YETU HAPA