Tuesday 4 August 2015

MWANAHARAKATI MASHUHURI APIGWA RISASI NCHINI BURUNDI


Mwanaharakati mashuhuri nchini Burundi amepigwa risasi na kujeruhiwa vibaya na mtu mwenye silaha aliyekuwa kwenye pikipiki.



Kwa mujibu wa familia yake mwanaharakati huyo Claver Mbonimpa ameshambuliwa katika Jiji la Bujumbura.



Mwanaharakati huyo ni miongoni mwa wakosoaji wakubwa wa rais Pierre Nkurunziza katika uamuzi wake wa kuwania urais kwa muhula wa tatu.



Siku ya jumapili msaidizi wa rais Jenerali, Adolphe Nshimirimana aliuwawa kwa kushambuliwa kwa risasi Jijini Bujumbura.

0 comments:

Post a Comment

OFFICIAL MEMBER

OFFICIAL MEMBER

Please Share This Site

HABARI ZETU

LIKE PAGE YETU HAPA