NDEGE ITAKAYOHISIWA KUWA NA UNGA RUKSA KUTUNGULIWA
BUNGE LAPITISHA SHERIA YA KUTUNGUA NDEGE ITAKAYOHISIWA KUWA NA UNGA
Baraza la Congress la Peru limeidhinisha muswada wa sheria ambayo inaruhusu vikosi vya anga vya taifa hilo kuitungua ndege yoyote watakayoihisi imebeba dawa za kulevya.
Peru huzalisha cocaine nyingi zaidi ya mataifa mengine duniani ambapo sehemu kubwa ya dawa hiyo ya kulevya huingizwa kwa magendo nchini Marekani.
Muswada huo umepitishwa bila kupingwa unangojea kutiwa saini na rais Ollanta Humala, ingawa unakabiliwa na upinzani kutoka Marekani kwa kukiuka usalama wa anga.
0 comments:
Post a Comment