Monday 28 September 2015

KIFO CHA MCHEZAJI COASTAL UNION,TFF YATUMA RAMBIRAMBI

Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini (TFF) limetuma salam za rambirambi kwa mwenyekiti wa klabu ya Coastal Union, Dr Twaha Ahmed kufuatia kifo cha mchezaji Mshauri Salim aliyefariki jana jioni jijini Tanga.
Katika salam hizo za Rais wa TFF Jamal Malinzi kwenda kwa uongozi wa klabu ya Coastal Union, amewapa pole wafiwa ndugu jamaa na marafiki pamoja na uongozi wa klabu hiyo na kusema TFF wako nao pamoja katika kipindi hichi cha maombelezo.

Marehemu Mshauri Salim alikuwa mchezaji wa kikosi cha vijana (U20) cha Coastal Union, alifariki jana jioni wakati akipelekwa hospitali baada ya kuanguka uwanjani wakati wa mchezo wa utangulizi wa timu yake dhidi ya timu ya Eagle Academy ya jiji humo.
Kabla ya umauti kumfika, Mshauri aligongana na mchezaji wa timu ya Eagle Academy na kutolewa nje kwa matibabu, ambapo aliweza kurudi uwanjani na kuendelea na mchezo huo kabla ya kuanguka peke yake tena uwanjani na kufariki akiwa njiani kupelekwa hospitalini.

0 comments:

Post a Comment

OFFICIAL MEMBER

OFFICIAL MEMBER

Please Share This Site

HABARI ZETU

LIKE PAGE YETU HAPA