UMEME WA PUMBA ZA MCHELE, MASHUDU YA PAMBA WATUMIKA KUENDESHEA MITAMBO YA TBL MWANZA
Meneja wa kiwanda cha Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) Mwanza, Raymond Richmond,akizungumza na waandishi wa habari kuhusu kampuni hiyo kutumia mapumba ya mchele na mashudu ya pamba,kama chanzo cha nishati ya umeme kinachotumika kuendeshea mitambo.Kushoto ni Meneja wa Maji na Nishati wa kampuni hiyo, Sunday Kidolezi.
Meneja wa kiwanda cha Kampuni ya Bia (TBL) Mwanza, Raymond Richmond, akizungumzia mradi wa matumizi ya mapumba ya mchele na mashudu ya pamba,ambacho ni chanzo cha nishati ya kuendesha mitambo kiwandani hapo.Nishati ni rafiki wa mazingira kwa sababu haina hewa ukaa.Wanaokoa Dola za Kimarekani (USD) 400,000 hadi 500,000 kwa mwaka ambazo zingetumika kununua mafuta mazito na dizeli ya kuendeshea mitambo.
Waandishi wa habari wakiongozwa na Meneja wa Kiwanda cha kampuni ya Bia (TBL) Mwanza, Raymond Richmond(wa kwanza kushoto), kwenda kutembelea mtambo unaotumia mapumba ya mchele na mashudu ya pamba kuzalisha nishati ya umeme inyotumika kuendesha mitambo ya kiwanda hicho.Kulia ni Meneja wa Maji na Nishati wa TBL, Sunday Kidolezi.
Meneja wa kiwanda cha Kampuni ya Bia (TBL) Mwanza,Raymond Richmod, akiwaonyesha waandishi wa habari, Daniel Mkate wa TRhe Guardian (nyuma) na Henry Kavirondo wa Chanel Ten,mashine inayosukuma mapumba ya mchele na mashudu ya pamba, kwenda kwenye mtambo wa kufua umeme unaotumika kuendesha mitambo ya kiwanda hicho.Kulia ni Meneja wa Maji na Nishati wa kampuni hiyo, Sunday Kidolezi.
Wafanyakazi wa kiwanda cha Kampuni ya Bia (TBL) Mwanza,wakijaza mapumba ya mchele kwenye mashine kwa ajili ya kuyasukuma kadi kwenye mtambo wa kuzalisha nishati ya umeme, unaotumiwa kuendesha mitambo ya uzalishaji ya kiwanda hicho.
Meneja wa Maji na Nishati wa kiwanda cha Kampuni ya Bia (TBL) Mwanza, Sunday Kidolezi, akifafanua jambo kwa waandishi wa habari kuhudu mradi huo wa uzalishaji wa nishati ya umeme,unaotumika kuendesha mitambo ya kiwanda cha kampuni hiyo kwa kutumia mapumba ya mchele na mashudu ya pamba.Wa kwanza kushoto ni Meneja wa kiwanda cha kampuni hiyo,Raymond Richmond.
0 comments:
Post a Comment