Monday 19 October 2015

OFISI YA MUFTI YAANDAA SEMINA KWA WAANDISHI WA HABARI PEMBA JUU YA UMUHIMU WA AMANI


MKUU wa kitengo cha fatwa kutoka afisi ya Mufti Pemba, sheikh Said Ahmad Mohamed, akitoa maelekezo kwenye semina ya waandishi wa habari ilioandaliwa na ofisi hiyo Zanzibar na kufanyika skuli ya sekondari Madungu Chake chake Pemba, (Picha na Haji Nassor, Pemba).
BAADHI ya waandishi wa habari walioshiriki semina ya siku moja ya umuhimu wa amani, ilioandaliwa na ofisi ya Mufti Zanzibar na kufanyika skuli ya sekondari Madungu Chake chake Pemba, (Picha na Haji Nassor, Pemba).
SHEIKH Thabiti Nouman Jongo kutoka afisi ya Mufti Zanzibar, akiwasilisha mada ya nafasi ya waandishi wa habari katika kutunza amani na utulivu, iliofanyika skuli ya sekondari Madungu Chake chake Pemba, (Picha na Haji Nassor, Pemba).
KATIBU wa Ofisi wa Mufti Zanzibar, Sheikh Fadhili Suleiman Soraga akifungua semina ya siku moja ya waandishi wa habari juu ya umuhimu wa amani, kulia ni sheikh Thabit Nouman Jongo na kushoto ni sheikh Abdurr-haman Abdalla nae kutoka afisi ya Mufti kisiwani Pemba, (Picha na Haji Nassor, Pemba).
MWANDISHI wa habari kutoka shirika la Magazeti ya serikali Zanzibar, kisiwani Pemba Haji Nassor, akichangia mada juu ya nafasi ya waandishi wa habari katika kuimarisha amani wakati na baada ya uchaguzi mkuu, kwenye semina iliofanyika. 

                                                                              Habari kwa hisani ya ZanziNews

0 comments:

Post a Comment

OFFICIAL MEMBER

OFFICIAL MEMBER

Please Share This Site

HABARI ZETU

LIKE PAGE YETU HAPA