KILI STARS KUPAMBANA TENA DHIDI YA ETHIOPIA KATIKA ROBO FAINALI SIKU YA JUMATATU
Wakati Stars imeingia robo fainali kama kinara
wa Kundi A, Ethiopia imetumia ‘mlango wa uani’ maarufu kama best looser baada
ya sare ya bao 1-1 dhidi ya Stars, leo.
Stars ilishinda mechi zake mbili za hatua ya
makundi na kutoka sare dhidi ya Ethiopia.
Mechi hiyo ya Jumatatu inatarajiwa kuwa ngumu
kwa kuwa Ethiopia ambao wameonyesha wazi hawana kikosi imara, watakuwa
wameongeza hali ya kujiamini baada ya sare hiyo iliyowavuja hadi robo fainali.
Hata hivyo, Kocha Mkuu wa Kili Stars, Abdallah
Kibadeni amesema ana imani na kikosi chake.
“Tulicheza vizuri, sema limetokea kosa na wao
wamelitumia kupata bao. Lakini tunakutana nao tena hatua ya robo fainali.
“Mechi itakuwa ngumu kwa kuwa wako nyumbani
kama wenyeji, lakini tutapambana kwa kuwa tumetumwa na Watanzania,” alisema.
0 comments:
Post a Comment