LIVERPOOL YAITWANGA CHELSEA 3-1, SASA MOURINHO ASOGEA MLANGO WA KUTOKEA
Kocha wa Liverpool akipongezana na beki Sakho |
Chelsea ilianza vizuri wakati Ramires akipachika bao la kuongoza baada ya dakika tatu tu bali imani ya
Liverpool haikupotea na a Philippe
Coutinho aliisawazishia kwa mkwaju maridadi katika kipindi cha kwanza mwishoni.
Baada ya mapumziko Coutinho tena aliiweka Liverpool
mbele kwashuti kali lililombabatiza John
Terry na dakika 16 baadae Christian Benteke alipachika bao la tatu na mpira
kumalizika kwa ushindi wa kocha Klopp ushindi ambao alistahili.
Ramires akishangalia baada ya kuipatia Chelsea bao la kuongoza |
Ushindi wa Liverpool unaongeza shinikizo kwa meneja wa Chelsea Jose Mourinho ambaye klabu yake imeshindwa kabisa kutamba msimu huu.
Matokeo kamili ya mechi za Jumamosi ni kama ifuatavyo:
Chelsea 1-3 Liverpool
Crystal Palace 0-0 Man Utd
Man City 2-1 Norwich
Newcastle 0-0 Stoke
Swansea 0-3 Arsenal
Watford 2-0 West Ham
West Brom 2-3 Leicester
0 comments:
Post a Comment