MAZISHI YA MAWAZO BADO KIZUNGUMKUTI. CHADEMA KUTINGA MAHAKAMANI
Na:George Binagi-GB Pazzo @BMG
Chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema kimesitisha shughuli za mazishi ya aliekuwa Mwenyekiti wa Chama hicho Mkoani Geita marehemu Alphonce Mawazo, baada ya jeshi la polisi Mkoani Mwanza kuzuia zoezi la kuuaga mwili wake lililokuwa limepangwa kufanyika juzi jumamosi Jijini Mwanza.
Chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema kimesitisha shughuli za mazishi ya aliekuwa Mwenyekiti wa Chama hicho Mkoani Geita marehemu Alphonce Mawazo, baada ya jeshi la polisi Mkoani Mwanza kuzuia zoezi la kuuaga mwili wake lililokuwa limepangwa kufanyika juzi jumamosi Jijini Mwanza.
Mwenyekiti
wa Chama hicho Taifa, Freeman Mbowe alibainisha hayo jana wakati
akizungumza na Wanahabari Mkoani Mwanza, ili kutoa msimamo wa Chama
baada ya kuwepo kwa mazungumzo baina yake na familia ya marehemu
Mawazo.
Alisema
kuwa baada ya mazungumzo hayo, Chadema pamoja na familia ya marehemu
Mawazo wamekubaliana kwenda Mahakama Kuu Kanda ya Mwanza kufungua shauri
la kuomba tafsiri ya Kimahakama juu ya zuio hilo la jeshi la polisi
kuzuia mwili wa marehemu Mawazo kuagwa Jijini Mwanza kabla ya Kwenda
kuzikwa Kijijini kwake Chikobe katika Wilaya ya Busanda Mkoani Geita.
Nae
Mchungaji Charles Lugiko ambae ni baba mlezi wa marehemu Mawazo, alisema
anasikitishwa na hatua iliyochukuliwa na jeshi la polisi ya kuzuia
mwili wa marehemu Mawazo kuagwa Jijini Mwanza ambapo ameeleza kuwa na
matumaini makubwa ya kwamba mahakama itatenda haki juu ya suala hilo.
Frederick
Sumaye pamoja na Edward Lowasa ambao ni Viongozi Waandamizi wa Chadema,
walisema hatua ya jeshi la polisi kuzuia mwili wa Mawazo kuagwa Jijini
Mwanza si sawa na kwamba inaweza kuwa chanzo cha uvunjifu wa amani.
Mwishoni
mwa wiki iliyopita, Jeshi la Polisi Mkoani Mwanza kupitia kwa Kamanda
wake Charles Mkumbo, lilizuia zoezi la mwili wa marehemu Mawazo Kuagwa
Jijini Mwanza, kwa madai kwamba limepokea taarifa za kiitelejensia za
kuwepo baadhi ya vikundi vya watu kutumia mwanya huo kufanya fujo na
hivyo kuhatarisha usalama wa raia na mali zao.
Aidha
Kamanda Mkumbo aliitaja sababu nyingine kuwa ni uwepo wa mlipuko wa
Ugonjwa wa Kipindupindu Mkoani Mwanza, ambao umesababisha jeshi hilo
kutoruhusu mikusanyiko ya aina yoyote inayoweza kusababisha ugonjwa huo
kuenea zaidi kwa mjibu wa wataalamu wa afya ambapo lilishauri zoezi la
kuaga mwili huo kufanyika Mkoani Geita ambapo mazishi ya marehemu Mawazo
yatarajiwa kufanyika.
Katika
uchaguzi uliomalizika hivi karibuni, marehemu Alphone Mawazo alikuwa
mgombea ubunge Jimbo la Busanda Mkoani Geita kupitia Chadema, akiwa pia
ni Mwenyekiti wa chama hicho mkoani humo ambapo aliuawa kikatili kwa
kukatwa mapanga na mashoka na watu wasiojulikana jumamosi iliyopita ya
Novemba 14 mchana huku kifo chake kikihusishwa na uhasama wa kisiasa.
0 comments:
Post a Comment