TANZIA: ALIYEKUWA MKURUGENZI MSAIDIZI WA SHUGHULI ZA BUNGE BI. HELLEN MBEBA AFARIKI DUNIA
Katibu wa Bunge Dkt. Thomas Kashililah, anasikitika
kutangaza kifo cha mtumishi wa Bunge, Bi. Hellen Stephen Mbeba (36), aliyekuwa Mkurugenzi
Msaidizi - Shughuli za Bunge, kilichotokea ghafla leo Ijumaa tarehe 27/11/2015 wakati
akipelekwa Hospitali ya Mkoa wa Dodoma kwa matibabu.
Msiba upo nyumbani kwake eneo la Kisasa, Mjini
Dodoma. Taarifa zaidi na taratibu nyingine ikiwa ni pamoja na ratiba kamili ya
maziko zitaendelea kutolewa na Ofisi ya Bunge kwa kushirikiana na familia ya
Marehemu pindi mipango itakapokamilika.
MUNGU AIWEKE ROHO YA MAREHEMU MAHALI PEMA
PEPONI, AMINI!
BWANA ALITOA, NA BWANA AMETWAA, JINA LAKE
LIHIMIDIWE!
Imetolewa na:
Kitengo cha Habari, Elimu na Mawasiliano
Ofisi ya Bunge
Dar es Salaam
27.11.2015
0 comments:
Post a Comment