Monday, 22 November 2021

RAIS SAMIA ATUNUKU KAMISHENI KWA MAAFISA WAPYA 118

.com/img/a/
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi, Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa katika picha ya pamoja na Maafisa wapya wa JWTZ katika Chuo cha Mafunzo ya Kijeshi Monduli TMA mkoani Arusha leo tarehe 22 Novemba 2021 baada ya kuwatunuku Nishani Maafisa hao.
.com/img/a/
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi, Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa katika picha ya pamoja na wahitimu wapya katika ngazi ya Shahada ya Sayansi ya Kijeshi katika masomo ya kiraia katika Mahafali ya pili ya Chuo cha Uhasibu Monduli Arusha leo tarehe 22 Novemba 2021.


Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Mh.Samia Suluhu Hassan ametunuku kamisheni kwa maafisa wanafunzi katika chuo Cha mafunzo ya kijeshi Monduli mkoani Arusha


Maafisa hao wapya ni kundi la 02/18-Shahada ya Sayansi ya kijeshi (BMS)idadi 61 ambao wamepata mafunzo miaka mitatu na kuhitimu shahada ya Sayansi ya kijeshi pamoja na kundi la 08/18 Jeshi la Anga idadi 56 waliopata mafunzo katika shule ya Anga ya kijeshi hapa Nchini


Aidha katika wahitmu hao kuna marubani wa ndegevita,Marubani na Wahandisi Ndege  huku waliopata kamisheni jumla yao ni 118,kati yao wanaume 99 na wanawake 19


Zoezi la kutunuku kamisheni kwa maafisa hao lilifanyika kwa mara ya kwanza na Rais na Amir Jeshi Mkuu tangu alipoapishwa kuwa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu na ni mara ya pili kutunuku kamisheni ambapo mara ya kwanza ilikuwa tarehe 17 April 2021 Ikulu jijini Dodoma


Kabla ya kutunuku kamisheni,Rais Mama Samia amekagua Gwaride lililoandaliwa na maafisa wanafunzi hao na baadae aligawa zawadi kwa wanafunzi waliofanya vizuri zaidi kwa kila kundi


Wakati huo huo  Rais Mama Samia alitunuku shahada ya kwanza ya Sayansi ya kijeshi kwa maafisa wapya 61


Mafunzo ya shahada hiyo yaliendeshwa katika chuo Cha  mafunzo ya kijeshi Monduli kwa kushirikiana na chuo cha Uhasibu njiro (IAA)


Sherehe hizo zilihudhuliwa na viongozi mbalimbali wakiwepo wakuu wa vyombo vya ulinzi na usalama ,wawakilishi wa nchi rafiki ,makamanda,walezi na wawazi wa maafisa wapya.


Picha na Ikulu


.com/img/a/.com/img/a/

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu, Mhe. Samia Suluhu Hassan akitunuku Kamisheni kwa Maafisa wanafunzi  kundi la 02/18 wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) katika sherehe zilizofanyika kwenye Chuo cha Mafunzo ya Kijeshi Monduli (Tanzania Millitary Academy - TMA) mkoani Arusha   leo tarehe 22 Novemba 2021.

.com/img/a/
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu, Mhe. Samia Suluhu Hassan, akimvalisha bawa 2lt. Ibrahim Joseph Mwamboli kuashiria kuhitimu kozi ya Urubani kati ya Maafisa wapya wanafunzi 56 wa JWTZ katika Chuo cha Mafunzo ya Kijeshi Monduli (TMA) mkoani Arusha leo tarehe 22 Novemba, 2021.

.com/img/a/
.com/img/a/
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu, Mhe. Samia Suluhu Hassan, akimvalisha bawa Slt. Asnat Rashid Akbar kuashiria kuhitimu  katika kozi ya Urubani kati ya Maafisa wapya wanafunzi 56 wa JWTZ katika Chuo cha Mafunzo ya Kijeshi Monduli (Tanzania Military Academy-TMA) mkoani Arusha   leo tarehe 22 Novemba, 2021.
.com/img/a/
.com/img/a/
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu, Mhe. Samia Suluhu Hassan, akitunuku Shahada ya Sayansi ya Kijeshi katika masomo ya kiraia kwa Wahitimu 61 wa JWTZ katika Mahafali ya pili ya Chuo cha Uhasibu yaliyofanyika TMA Monduli mkoani Arusha leo tarehe 22 Novemba, 2021.
.com/img/a/

.com/img/a/
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu, Mhe. Samia Suluhu Hassan, akifunga mafunzo kwa wahitimu wapya katika ngazi ya Shahada ya Sayansi ya Kijeshi katika masomo ya kiraia kwa Wahitimu 61 wa JWTZ katika Mahafali ya pili ya Chuo cha Uhasibu yaliyofanyika Monduli mkoani Arusha leo tarehe 22 Novemba 2021.
.com/img/a/
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu, Mhe. Samia Suluhu Hassan, akizungumza na Mkuu wa Itifaki wa JWTZ Kanali Kobero wakati wa Mahafali ya pili ya Chuo cha Uhasibu yaliyofanyika TMA Monduli mkoani Arusha leo tarehe 22 Novemba, 2021.


.com/img/a/

.com/img/a/

.com/img/a/

.com/img/a/

.com/img/a/

.com/img/a/

.com/img/a/

0 comments:

Post a Comment

OFFICIAL MEMBER

OFFICIAL MEMBER

Please Share This Site

HABARI ZETU

LIKE PAGE YETU HAPA