Tuesday 8 March 2022

ABOUT LOVE# SIRI 9 ZA KUWA NA UHUSIANO IMARA NA WENYE KUDUMU ZAIDI...CHECK OUT

MAHUSIANO: NAMNA YA KUONGEA WAKATI WA UTONGOZAJI, ILI KUMTONGOZA MWANAMKE KWA MAFANIKIO ZAIDI.
 Nakusalimu wewe msomaji wa FUNGUKA LIVE
 kuelekea mwisho wa mwaka naamini umekutana na kupitia mambo na changamoto mbalimbali katika ishu hii ya mahusiano ya kimapenzi. Kama yalikuumiza "Pole" na kama umepata faraja "Hongera" yote ni sehemu ya maisha lakini kubwa mshuruku Mungu kwa zawadi ya uhai.


Leo ninmeguswa nikushirikishe  njia hizi 9 ambazo zitajenga na kuupa afya uhusiano wako. Sitaki kukuaminisha kwamba ni HIZI PEKEE la hasha!! lakini kila jambo lina msingi ukizingatia majibu yake utayaona na hatajuta kuutumia muda wako kusoma.



01. Usiwaache Rafiki zako
Ni dhahiri kwamba unataka mchumba wako ndio awe wa kwanza kupata habari nzuri pale inapotokea au mtu wa kwanza kufuta machozi yako pale unapopata shida lakini mara nyingine utamuhitaji rafiki yako hasa kwa wanawake kuna vitu ukimwambie mchumba wako hawezi kukuelewa lakini ukijadiliana na rafiki yako wa kike anaweza kukusaidia na kukupa ushauri.

02. kukua
kukua na kubadilika kama wewe kutafanya mahusiano yenu kuwa bora zaidi. Moja ya vitu muhimu kabisa katika mahusiano ni kujifunza kuhusiano na wewe mwenyewe zaidi au sawa na utakavyojifunza kuhusu partner wako. Kwa kuangalia vitu unavyofanya ukiwa na partner wako na jinsi anavyokuletea changamoto itakufanya na wewe ukue kilazima.

03. Msisahau Mlianzaje
kumbukeni mlivyoanza , jinsi mapenzi yalivokua , hata kama mmeishi kwa miaka mitano pamoja msiache zile hisia za mwanzo zikaondoka. Fanya juhudi za kuwa mbunifu na mshangaze mwezio.

04. Omba ruhusa kuongelea jambo fulani
Simaanishi uombe kwa unyonge bali pale unapotaka kuzungumza na mwezako kuhusu jambo lilalogusa sana maisha yenu ni vizuri kuuliza kwanza kama ni wakati sahihi.

05. Onesha Shukrani
kila mtu hapendi kuonekana yupo chini lakini kumshukuru mwenzako kwa safari aliokupeleka mbuga za wanyama au pesa za matumizi alizokupa kutamfanya asione kwamba unamchukulia poa na kutamfanya aendelee kukudhamini na kukuzidishia mambo mazuri.

06. Ongeza vitu vipya katika mahusiana
Ile safari ya kwenda wote kwa mara ya kwanza zanzibar au kujifunza kozi mpya basi ni vyema kuvifnya vitu hivi vipya pamoja. Ni vyema kukua pamoja , na kupeana changamoto pamoja mkiwa na uzoefu mpya mlioupata pamoja. 



07. Bishaneni lakini kwa jambo maalumu
ule mpango wa kukusanya malalamiko kibao ya mwezi wako mfano pale mnapogombana kuhusu kuchelewa on a date then mnaanza kuongezea na vitu vingine kibao kama kutompigia simu , kutovaa vizuri , kutokujali na mengine kibao.Kubishana kuhusu mambo mia kwa wakati mmoja ni vigumu kukabiliana nako hivyo bishaneni mara moja jambo linapotokea. 



08 . Panga Quality time na partner wako
Hasa uhusiano unapozidi kukua ni muhimu kuwa na muda wa pekee ambao mtazungumza kuhusu uhusiano wenu pekee na mipango muhimu ya baadae.Sio kila muda mpo wote mmegandana hampumui.  


NAOMBA UELEWE  Uhuru ni muhimu lakini pia kazi ni muhimu pia kwa hiyo peaneni nafasi kila mmoja aweza kufanya yake,amtafakari mwenzake na pia AMMISS mwenzake. 


09. Kuelezea Hisia
Moja kati ya msingi wa kuwa na mahusiano imara ni uwezo wa kuonesha hisia zako kwa partner wako na kujua kumsikiliza.kusema “nimekuelewa” haimaanishi “nimekubaliana na wewe” hivyo ni vema kumsikiliza mwenzio kuliko kukubali kila kitu ilimradi kuwe na amani.



 Nakusihi uelewe kuwa changamoto ni lazima na muhimu PLAY YOUR PART na hutakuwa wa kulaumiwa kamwe.



NAKUTAKIA MAANDALIZI MEMA KUELEKEA MWISHO WA MWAKA  2016

*Kd Mula*

0 comments:

Post a Comment

OFFICIAL MEMBER

OFFICIAL MEMBER

Please Share This Site

HABARI ZETU

LIKE PAGE YETU HAPA