HATIMA YA KAGAME KUAMULIWA KWA KURA YA MAONI
Rais Paul Kagame wa Rwanda.Rwanda sasa itapiga kura ya maoni katika kipindi cha wiki ijayo juu ya mabadiliko ya katiba kumruhusu Rais Paul Kagame kuwania muhula wa tatu wa kuiongoza nchi hiyo, serikali ya nchi hiyo imetoa tamko .
Kufuatia mabadiliko hayo ya kikatiba, kuna uwezekano wa rais Paul Kagame kusalia madarakani mpaka kufikia mwaka 2034.
Kwa mujibu wa serikali, wanyarwanda waishio ughaibuni watapiga kura Disemba 17, na siku inayofuata ndio watapiga kura wanyarwanda waishio nchini Rwanda.
Hata hivyo, jaribio hilo limekwisha kulalamikiwa na nchi za umoja wa ulaya ikiwemo Marekani ambayo imemtaka Rais Kagame kuwa mfano wa kuigwa katika Ukanda wa Maziwa Makuu kwa kuachia madaraka mwishoni mwa utawala wake ambao unafikia kikomo mwaka 2017.
Naye rais Paul Kagame ameijibu kauli hiyo kwa kutaka mataifa mengine kuacha kuingilia masuala ya ndani ya nchi za Afrika Mashariki.
Baraza la Senet nchini humo limeshatoa baraka zake kwa muswada huo wa mabadiliko ya katiba mwezi uliopita na kumruhusu Kagame kugombea tena nafasi hiyo mnamo mwaka 2017.
Wakati mabadiliko mengine tarajiwa ya kufupisha muda wa utawala kwa miaka 7 hadi 5 na kuweka ukomo wa madaraka kwa vipindi viwili tofauti, sheria hiyo haitakuwa na nguvu mpaka kufikia mwaka 2024, hapo tena Rais Paul Kagame ataweza kugombea kwa awamu mbili tofauti za miaka 5.
Mabadiliko hayo yanatabiriwa kupitishwa bila upinzani wowote kwa kumpa rais Kagame kura ya ndio.
Chama cha Paul Kagame cha Patriotic Front, kilikomesha mauaji ya kimbari yaliyotokia nchini humo mnamo mwaka 1994 na kukitoa madarakani chama cha Wahutu wenye msimamo mkali.
Katika mauaji hayo ya kimbari inakadiriwa kuwa wa Tutsi laki nane waliuawa.
Rais Kagame mpaka sasa hajathibitisha kama atagombea tena nafasi hiyo mnamo mwaka 2017 kama atapewa ridhaa, ingawa ameahidi kutoa maamuzi yake ya endapo atagombea ama la baada ya kupigwa kwa kura ya maoni.BBC
0 comments:
Post a Comment