WATUMISHI WAANDAMIZI SABA WA TANESCO WAFUKUZWA KAZI KWA TUHUMA MBALIMBALI
Mkurugenzi
Mkuu wa Tanesco, Felschimi Mramba akizungumza na waandishi habari juu
ya mikakati mbalimbali ya uzalishaji umeme katika mazungumzo
yaliyofanyika leo jijini Dar es Salaam, Kulia ni Kaimu Naibu Mkurugenzi
Mtendaji (Uzalishaji na Huduma kwa Mteja), Mhandisi Sophia Mgonja,
Kushoto ni Kaimu Naibu Mkurugenzi Mtendaji Uzalishaji Umeme, Nazir
Kachwamba, kushoto kutoka kulia ni Meneja Uhusiano Adrian Severine.
Waandishi habari wakimisikiliza Mkurugenzi Mkuu wa Tanesco, Mhandisi Felschimi Mramba leo jijini Dar es Salaam.
Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii.
SHIRIKA
la Umeme nchini (Tanesco) limewafukuzisha kazi watumishi waandamizi wa
Tanesco upande wa maneja na wahasibu kutokana na ubadhirifu wa fedha
katika utumishi wao.
Akizungumza
na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi Mkuu wa
Tanesco, Felschimi Mramba amesema kuwa shirika halitaweza kuwaacha
watendaji wakawa wanafanya kazi kwa rushwa wakati wanalipwa mishahara.
Amesema
wataendelea kuchukua hatua kwa watendaji wote watakabainika kufanya
udanganyifu au kutoa lugha zisifaa kwa wateja na wakati mwingine kuomba
fedha kwa huduma ambazo ni haki ya mwananchi kupata.
Mramba
amesema Tanesco imeongeza uzalishaji wa umeme unaotumia gesi megawati
300 sawa na asilimia 115 na kufanya kuwa na umeme wa uhakika huku
miradi mingi ikiendelea kufanyika.
Amesema
wanatarajia kupata megawati 240 kutoka Kinyerezi namba mbili wakati
wowote na kufanya shirika kuwa na umeme wa uhakika.
Aidha
amesema wakati wa suala miundombinu likifanyiwa kazi wananchi wawe
wavumilivu wa kukatika umeme katokana na kuboresha miundombinu hiyo.
Aliongeza
kuwa wanaotaka kufanya kazi na Tanesco kwa kupata nguzo lazima
wazalishe nguzo zenye ubora wa kuweza kuhimili kwa muda mrefu bila
kuanguka kuanguka.
0 comments:
Post a Comment